-->

Header Ads

BREAKING: AJALI NYINGINE DUMILA MOROGORO YAACHA MASWALI


Ikiwa bado watanzania tukiomboleza kutokana ajali ya jana mkoani Arusha iliyoondoka na wanafunzi 32, na kuacha majonzi kwetu na TAIFA ZIMA.
Habari za hivi punde toka Morogoro Dumila
Eneo la Kutoka mvomelo ukipita matuta ya mwanzo kabla hujafika Makunganya   kuna Gari ya abiria aina ya Eicher imegongwa na lori na inariportiwa kuwa hali mbaya sana.. Bado hakuna ripot ya kifo wala majeruhi
@afande Anna Job kajulishwa  
Tumwombe  Mungu atupiganie

Tarifa kamili baada ya muda mfupi ujao.. Tayari AKISI TV iko njiani kuelekea eneo la tukio kukupa habari zaidi.

Pia Tunarajia kupata taarifa kamili kutoka  jeshi la polisi.

......................................................................
UPDATES 

 Watu 10 wamejeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, watatu kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la kampuni ya Karim walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.
Walikuwa wakitoka Turiani kwenda Morogoro ndipo basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Morogoro kwenda nchini Rwanda.
Walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea saa sita mchana eneo la Ranchi ya Dakawa wakati dereva wa lori alipojaribu kuyapita magari mawili bila ya kuchukua tahadhari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema majeruhi walikuwa 24 na baada ya kufikishwa hospitali wengine walitibiwa na kuruhusiwa na waliolazwa ni 10, watatu wakiwa na hali mbaya.
Alisema dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi.

No comments

Powered by Blogger.