NDEGE ZA KIVITA ZARINDIMA ANGA LA KOREA
Taarifa kutoka vyombo vya usalama vya Korea Kusini zinasema kuwa ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.
Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kutatanisha kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini.
Hatahivyo Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.
Hapo awali Trump amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.
Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya White House alisema baadaye kwamba mazingira kama hayo, yanayoweza kufanikisha mkutano wa Trump na Kim hayapo.
Hatika hali hiyo Korea Kaskazini imeongeza kasi katika majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia miaka ya karibuni licha ya marufuku ya Umoja wa Mataifa.
Korea Kaskazini inahofia kwamba Marekani na Korea Kusini wanaweza kutumia nguvu kumuondoa madarakani Kim Jong-un.
Jumatatu, Japan ilituma meli ya kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya kwanza ya aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata iliyowezesha taifa hilo kuanza kupanua uwezo wa jeshi lake.
No comments