MATOKEO YA MICHEZO YA LIGI KUU VODACOM LEO JUMAMOSI 7 MAY 2017
AKISI TV inakuletea matokeo ya mechi zilizochezwa siku ya leo Jumamosi
Michezo Ligi Kuu Tanzania Bara iliendelea siku ya jana Jumamosi, kwa mechi tano kupigwa kwenye viwanja tofauti tofauti
Kama ilivyo ada, Goal inakuletea matokeo ya mechi zilizo chezwa siku ya Jumamosi
Yanga 2-0 Tanzania Prisons
Klabu ya Yanga imefanikiwa kukamata usukani kwa kufikisha pointing 59 baada ya kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya Prisons
Magoli ya kipindi cha pili ya Mrundi Tambwe na Chirwa yametosha kuipa Yanga alama tatu muhimu huku Prisons wakibaki na alama zao 31 tofauti ya pointi 4 kwenye nafasi ya kushuka daraja
Majimaji 3-0 Mwadui
Majimaji ya Songea wamefufua matumaini ya kubakia Ligi Kuu msimu ujao baada ya ushindi mnono ya goli tatu kwa bila, magoli ya Kelvin Sabato, Peter Mapunda na Iddy Chipwagile
Kwa ushindi huo kumeifanya Majimaji kufikisha alama 29 kwenye msimamo
Toto African 2-1 JKT Ruvu
Rasmi klabu ya JKT Ruvu imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kukubali kipigo cha goli mbili kwa moja dhidi ya TOT0, magoli mawili ya mshambuliaji Wazir Junior yalitosha kuipa ushindi TOTO na kufufua matumaini kwa klabu hiyo ya kuepuka kushuka daraja
Azam 3-1 Mbao FC
Klabu ya Mbao Fc ya jijini Mwanza imejiweka kwenye mazingira magumu ya kushuka daraja baada ya kupokea kipigo cha goli tatu kwa moja na Azam
Waoka mikate wa Azam wameendelea kukamatia nafasi ya licha ya ushindi huo mzuri wa magoli matatu kwa moja, shukrani kwa washambuliaji Shabani Iddi aliyefunga mawili na John Bocco
No comments