BODI YA MIKOPO NA SAKATA LA KUKIUKA SHERIA YA UTOAJI WA FEDHA ZA MAFUNZO KWA VITENDO.
BODI YA MIKOPO YAKIUKA SHERIA YA UTOAJI WA FEDHA YA MAFUNZO KWA VITENDO.
Mtandao wa wanafunzi Tanzania TSNP.kupitia idara yake ya haki na wajibu wa wanafunzi, inadai imesikitishwa na kitendo cha bodi ya mikopo kukeuka sheria ya utoaji wa fedha za mafunzo kwa vitendo mwaka 2016/2017,
Kaimu mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa wanafunzi -TSNP.,Mr. Abdul Omary Nondo.anasema kuwa Bodi ya mikopo wamekeuka sheria baada ya kutoa mgawanyo wa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 2016/2017,kwa mgowanyo wa "Means testing" jambo ambalo sheria na muongozo wao hausemi hivyo,3.6 katika muongozo wao inasema fedha ya Mafunzo kwa vitendo itatolewa kwa siku 56 ,kila siku sh.10000 sawa na sh.560000.na elf 60 ya nauli sawa na 620000.ambapo sheria hiyo hiyo inasema fedha ya mafunzo kwa vitendo hazitatolewa tofauti tofauti kwa kila mwanafunzi ila ni wote sawa.
Huu juu ni muongozo wa bodi mwaka 2016/2017,unaokataza kugawanya fedha za mafunzo kwa vitendo,ambapo hadi sasa ni jambo la kushangaza muongozo huu haupo katika tovuti yao wameutoa anasema kaimu mkurugenzi idara ya haki za wanafunzi-TSNP, abdul nondo.
Pia Abduli nondo anaendelea sema kuwa wanafunzi wanaotarajia kwenda mafunzoni mwezi wa saba,wamepewa pungufu ya mgawanyo unaotakiwa.kuna wanafunzi wamepewa hadi sh.55000 kwa siku 56.
Abduli nondo anasema"mtandao wa wanafumzi TSNP" hatujaridhishwa na ukeukaji wa sheria unaofanywa na bodi ya mikopo ,hivyo lazima tuseme na kuwasemea wanafunzi ili yanayotokea yasiendelee kutokea,na tunasema kwa sababu wazazi na jamii ijue kuwa watoto wao wanapoelekea katika mafunzo kwa vitendo wamepewa fedha pungufu ambayo haita wasaidia saana bali watapata taabu huko waendako"
Pia Abduli Nondo amesema kwa kushirikiana na wanasheria wa mtandao ndugu,Rayson Elijah,bob chacha wanaangalia namna ya kulisemea suala hili kwa nguvu ili haki za wanafunzi zisiwe zinakeukwa kwa kutofuata sheria inayoongoza.ingawa sio wanafunzi wote wanaopata mkopo,ila hao ambao wanapata ni vizuri wakapata bila kukeuka sheria.
Pia amesema tayari ameanza kufanya mawasiliano na viongozi wa wanafunzi kupitia wizara ya mikopo vyuo tofauti tofauti kuangalia namna gani jambo hili linaweza kufikishwa sehemu husika na kukutana na uongozi wa bodi ya mikopo na wizara ya elimu kuona namna gani suala hili linaweza kutatuliwa.
Ili kuhakikisha wanafunzi wanatimiza majukumu yao ya kitaaluma kama inavyo takiwa,na mtandao wa wanafunzi Tanzania tunaendelea kufuatilia suala hili ngazi kwa ngazi na kwa utaratibu wote unao shahili amesema abdul nondo ambaye ni kaimu mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa wanafunzi-TSNP.
No comments