-->

Header Ads

MAMBO MATATU MUHIMU ALIYOTETA JACOB ZUMA NA RAIS MAGUFULI LEO


1. Rais John Magufuli amesema wamekubaliana na Rais Jacob Zuma kupeleka walimu kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufundisha Kiswahili.

Amesema yeye na Rais Zuma wameshakubaliana kuhusu hilo na kwamba walimu hao watakwenda nchini humo baada ya taratibu muhimu  kukamilika.


2. Rais John Magufuli amemshukuru Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwa mchango wa madawati uliotolewa na Serikali yake wakati wa kampeni za kuchangia madawati.

Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo (Alhamisi) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Amesema Serikali ya Afrika Kusini ambayo imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania ilikuwa miongoni mwa wachangiaji wa madawati wakati wa kampeni hiyo.

Kutokana na mchango wa madawati zaidi ya 1,000, Rais Magufuli amemshukuru Zuma akisema nchini hizo mbili zitaendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

 



3.Rais John Magufuli amemwomba Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini,ampigie debe kwenye jumuiya ya BRICKS kwa ajili ya kupata  mkopo wa kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Morogoro hadi Dodoma.
Rais Magufuli ambaye hakutaja kiasi cha mkopo huo, ametoa ombi hilo leo (Alhamisi) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Amemwambia Rais Zuma kuwa hivi sasa Serikali ya Tanzania ina fedha za kujenga reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, hivyo fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya kuendeleza ujenzi kutoka Morogoro hadi Dodoma.
Rais Magufuli amesema anaamini Serikali ya Afrika Kusini itasaidia ombi hilo kwa kuwa ni mwanachama mzuri wa jumuiya hiyo na pia Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa na historia nzuri .


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.