KUMBE ALIJITAKIA MWENYEWE!! Naibu Waziri Aliyetishiwa bunduki, Afikishwa Mahakamani Kisutu
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, na Mbunge wa Mkuranga, Adam Kighoma Ali Malima amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo akituhumiwa kumzuia Polisi kutekeleza majukumu yake.

Polisi hao walikuwa wameambatana na maofisa wa kampuni moja ambayo ni wakala wa kukusanya madeni, kukamata teksi bubu pamoja na kukamata magari ambayo yanaegeshwa sehemu ambayo si sahihi kisheria.
Licha ya Malima kuelezwa ukweli kuwa hakuwa ameegesha gari sehemu sahihi, lakini alikataa kulipeleka alikoambiwa jambo lililoibua mtafaruku mkubwa.
Baada ya kufikishwa mahakani yeye na dereva wake, wameachiwa kwa dhamana ya TZS milioni 5.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments