KIASI CHOTE KILICHOTUMWA NA SERIKALI KWA WAZAZI WA WATOTO ARUSHA HIKI HAPA..
Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,imetuma Sh 44.9 milioni kwa wazazi wa majeruhi ya ajali ya Lucky Vicent wanaotibiwa hospitali ya Mercy iliyopo Marekani
Watoto wanaotibiwa Marekani ni Saidia Ismail, Wilson Tarimo na Doreen Mshana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuna sababu ya kuelekeza nguvu kubwa kwa kuwasaidia majeruhi hao watatu walioponea chupuchupu kwenye ajali ya gari huko Karatu.
Pia alisema pesa hizo walizotuma zitaenda kusaidia familia zilizoondoka na majeruhi kwenda nchini Marekani na kwamba kila mzazi atapata Sh 11 milioni ,huku daktari aliyeondoka na majeruhi hao pamoja na muuguzi watapata Sh 5.5 milioni kila mmoja
"Tumetoa pesa hizo kwa familia zilizopo huko nchini Marekani ili ziweze kuwasaidia waliko huko ugenini," amesema Gambo
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa alisema fedha hizo zilizotolewa zinatokana na rambirambi zinazoendelea kuchangwa na wadau mbalimbali na ambako mpaka Mei 20 , Sh 67.99milioni zilipatikana.
Amesema pamoja na kutoa Sh 44.72 milioni,fedha zilizobaki ofisini kwake ni Sh 23.27 milioni na akasema fedha hizo zitaendelea kuwekwa huku timu ya wawazi wanne walioteuliwa na wafiwa wakiendelea kushirikiana na Serikali kuhakiki mapato na matumizi wa rambirambi hizo
"Kuna tuhuma nyingi ambazo zinadai rambirambi za wafiwa hazijawafikia wafiwa,taarifa hizo hazina ukweli,ofisi yangu imeratibu zoezi hilo kwa uaminifu wa hali ya juu na taarifa ya jumla imetolewa kwa umma juu ya mapato na matuzi yote," amesema Gambo
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments