-->

Header Ads

ILIVYOKUWA AJALI YA BASI UTURUKI KUUWA WATU 20 PAPO HAPO



Watu 20 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi moja la watalii kuanguka kutoka juu ya mwamba karibu na eneo la kujivinjari lililopo Kusini mwa Uturuki.

Watu wengine 11 walijeruhiwa wakati dereva alivyopoteza mwelekeo wa basi hilo dogo na kugonga kizuizi.

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimesema kuwa hakuna watalii wa kigeni waliokuwemo katika basi hilo.

Takriban watu 400 walikuwa wameabiri basi hilo kulingana na gavana wa mkoa wa Mugla, Amric Cicek ambaye anasema huenda breki zilifeli.

Lakini Meya wa eneo la Marmaris, Ali Acar aliambia gazeti la Uturuki la Hurriyet akisema  ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya dereva.

Vyombo vingine vya habari vinasema kuwa waathiriwa wengi walikuwa wanawake na watoto.



R.TEHRAN


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.