-->

Header Ads

HIMID MAO ASHATUA DENMARK TAYARI KUICHEZEA RANDERS FC

Kiungo wa Klabu ya Azam FC, Himid Mao tayari amewasili nchini Denmark kwenye makao makuu wa klabu ya Randers inayoshiri Ligi Kuu nchini humo ambako amekwenda kufanya majaribio.

Kama anavyoonekana hapo kwenye picha, akiwa katika uwanja unaotumiwa na timu hiyo unaoitwa ‘BioNutria Park Randers’.

Kwa mujibu wa tovuti ya timu hiyo, inaeleza kuwa Himid atafanya mazoezi na kikosi kingine cha vipaji cha Randers leo na kesho Jumatano kabla ya Ijumaa kujumuika na timu kubwa ya Randers.

Taarifa hiyo ya Randers inasema kuwa, Himid mbali na kufanya mazoezi atakuwa ni sehemu ya kikosi cha wachezaji wa akiba wa Randers kitakachocheza dhidi ya AC Horsens Jumanne ijayo kwenye Ligi ya Wachezaji wa Akiba ya nchini humo.

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA

No comments

Powered by Blogger.