BREAKING: MWENYEKITI CCM AUWAWA KIBITI
Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne Iddy Kirungi liliopo katika kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wilayani hapa ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwake.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.
Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.
Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.
Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.
Alisema majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana.
CREDIT; MWANANCHI
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments