NINI CHANZO CHA AJALI ARUSHA?
Kaimu mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa wanafunzi Tanzania- mtandao wa wanafunzi Tanzania(TSNP) Abdul omary Nondo,amesema mtandao wa wanafunzi ulistushwa saana na taarifa hii ya ajali iliyopoteza takribani wanafunzi 32,na walimu wao 2,na dereva.ni ajali kubwa saana kuwahi kutokea sababu tumepoteza wanafunzi wengi kwa wakati mmoja,ambao walikuwa na malengo makubwa ya kujenga taifa lao,hayo ameyasema leo katika kipindi cha daraja kinachorushwa na magic fm kila j.mosi
"suala sio kukataza safari zisiwepo ,jambo la msingi ni kujua chanzo cha ajali iliyotokea na zinazoendelea kutokea chanzo nini ili tuchukue hatua, amesema abdul nondo.
Pia anaendelea kusema kuwa lazima kufanyike ufuatiliaji mkubwa juu ya upatikanaji wa madereva hawa katika hizi shule ,trafiki polisi wajikite saana kukagua leseni za madereva hawa,kama anasifa zote za kuendesha gari kwa kufuata sheria za barabarani.na wajibu huo usichwe katika mikono mwa uongozi wa shule.
Ukaguzi wa magari mara kwa mara,magari mengine sio mazima,mabovu hayakidhi ila yanaachwa kubeba wadogo zetu,jambo ambalo ni hatari saana .
Idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kupanda gari izingatiwe kumekuwa na mchezo magari ya wanafunzi yanawajaza wanafunzi bila kuangalia idadi mfano kwa mujibu wa mkuu wa polisi charlse mkumbo mkoa wa arusha, alisema gari lile linatakiwa beba wanafunzi 30 tuu,kwa idadi ila ilizidisha ikabeba 38,lazima uangalifu ufanyike katika idadi.na sio kuwarundika kama magunia.
Pia uvaaji wa mikanda(seatbelt) wanafunzi wengi hawaangaliwi katika kuvaa mikanda wanapakiwa tuu,mfano katika ajali hii ya Arusha,gari lile lilibondeka mbele hii inamaana kuwa wanafunzi hawakuwa wamevaa mkanda ndio maana madhara yametokea makubwa kama wangevaa madhara mengi yasingetokea,inaonesha walirushwa mbele na kugongana hivyo mamlaka husika iangalie suala hili kwa umakini wa hali ya juu.
Abduli nondo ,anaendelea sema kuwa magari ya kubebea wanafunzi yanapaswa yafanane yote ili yatambulike kwa urahisi ya arusha mengi ni ya njano iwe hivyo tanzania nzima,yawe ya njano.
Ameongezea pia mamlaka husika Sumatra,trafiki polisi kuwashughulikia makondakta wote
wanaonyanyasa wanafunzi katika magari pindi waendapo shuleni,haifai hata kidogo,sheria mwanafunzi anatakiwa alipe sh.200/=ila kondakta anawafukuza wanafunzi wasipande,au hata wakipanda anawatolea maneno makali.amesema abduli nondo,kaimu mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa wanafunzi (mtandao wa wanafunzi tanzania TSNP).
Abdul nondo,amesema tayari mtandao wa wanafunzi tanzania umeandaa mapendekezo juu ya kipi kifanyike ili wanafunzi waepukane na ajali hizi,mapendekezo hayo yatatumwa wizara ya elimu,sumatra,na kitengo cha usalama barabarani makao makuu.
No comments