-->

Header Ads

HUYU NDIE JAGUAR KUTOKEA BIASHARA, MUZIKI HADI SIASA

Charles Njagua "Jaguar" amepewa ushindi na chama cha Jubilee na kumfanya kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Starehe. Jagua ameshinda rufaa aliyokata dhidi ya mbunge anayemaliza muda wake kwa madai alifanyiwa magumashi yeye na watu wake.

Mwanamuziki huyo atachuana na mwanaharakati Boniface Mwangi pamoja na Steve Mbogo. Jaguar ni mfanyabiashara pamoja na mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa akihesabiwa miongoni mwa wasanii wenye utajiri mkubwa kwa Afrika Mashariki.

Endapo atashinda uchaguzi hapo Agosti, Jaguar ataungana na wasanii wengine wa Afrika Mashariki kama Profesa Jay na Joseph Mbiliny "SUGU" kuingia bungeni. Muangalie Jaguar akihutubia wafuasi wake mara baada ya kutangazwa mshindi.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.