"MIKEKA" YAMPOZA MCHEZAJI, AFUNGIWA MIEZI 18.
LANCARSHIRE,Uingereza
Kiungo wa Burnley Joey Barton amefungiwa kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 18 baada ya kukiri kushiriki kucheza mchezo wa kubashiri matokeo (kamali) mara 1, 260 katika kipindi cha miaka10.
Adhabu hiyo inaungana na faini ya Euro 30, 000 na kutokushiriki wala kujishungulisha kwenye mambo yanayohusu soka mpaka atakapomaliza kifungo chake.
Chama cha soka nchini Uingereza (FA) kimetoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha na uchunguzi uliofanywa na kamati huru kuhusu tuhuma hizo.
Taarifa kutoka FA zimesema kuwa Machi 26, 2006 hadi Mei 13 mwaka jana mchezaji huyo amekuwa akishiriki mchezo huo na kuvunja kanuni ya FA namba E8.
Barton anakusudia kukata rufaa kuhusu ukali wa adhabu hiyo kwani anaamini maamuzi hayo yanamlazisha kustaafu soka kutokana na umri wake kuwa mkubwa huku akitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja na miezi sita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ameushukuru uongozi wa Burnley na mashabiki wake kwa kumuamini na kumtia moyo katika kipindi chote ambacho walikuwa pamoja kwani aliitumikia vyema timu hiyo kwa moyo wote.
No comments