-->

Header Ads

TAZAMA MAUAJI YA BARCELONA KWA OSASUNA

Miaka saba ya ukame wa goli imeisha leo kwa Javier Mascherano baada ya kupiga tuta safi lililoiandikia Barcelona goli la sita kwenye ushindi wa 7-1 dhidi ya timu ya Osasuna.
Tangu ahamie Barcelona akitokea klabu ya Liverpool, Mascherano hajawahi kucheka na nyavu akiwa na Barca licha ya kucheza mechi 319 katika michuano yote.

Licha ya goli la Mascherano kuonekana kama kichekesho mitandaoni, goli hilo limekua la 100 kwa Barcelona msimu huu huku pia likiwa goli la 300 tangu Luis Enrique aanze kuifundisha Barca.
Ushindi wa Barcelona ulitimizwa na magoli ya Lionel Messi, Andre Gomez na Fransisco Alcarer; wote walifunga mabao mawili kila mmoja. Tumekuwekea video nzima ya magoli ya pande zote mbili.


 

 JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.