-->

Header Ads

BREAKING NEWS: WAFUASI WA LIPUMBA WAVAMIA MKUTANO WA MAALIM SEIF HOTELINI LEO




UVAMIZI : Inaripotiwa kwamba kuna uvamizi umefanyika katika hoteli ya Vinna iliyopo Mburahati - Dar es Salaam ambapo kulikuwa na 'press conference ' ya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Wananchi ( CUF ). Wanachama hao ambao wanamuunga Mkono Maalim Seif, waliitisha mkutano na waandishi wa habari lakini mkutano huo ulivamiwa na watu wenye mapanga na mmoja mwenye bastola.
31m
 Inasemekana kwamba watu waliovamia mkutano wa wanachama wa  CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif ni kutoka upande unaomuunga mkono Prof Lipumba.

Walipovamia mkutano huo waliwashambulia wazungumzaji na baadhi ya waandishi habari waliokuwepo ndani ya chumba cha Mkutano. Pia waliwazuia kutoka nje hadi pale wananchi wa eneo hilo walipofahamu kinachoendelea na kuanza kupiga kelele.



Wavamizi walikimbia lakini mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa mmoja ( anayeonekana pichani ) wao amekamatwa na kushmbuliwa na Wananchi wa eneo hilo.

 Awali, walioitisha mkutano katika hoteli ya Vinna, walieleza kwamba lengo lao ilikuwa kueleza juu za ziara ya Maalim Seif. Walieleza kwamba wanataka kutoa onyo kwa wafuasi wa Prof Lipumba kwamba wasijaribu kukwamisha ziara ya Maalim Seif na pia walisisitiza kwamba Prof Lipumba aachie ofisi ya Uenyekiti wa CUF. .

 AKISI TV iko katika eneo hilo na tutakuletea taarifa zaidi



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.