-->

Header Ads

SABABU KUU SABA ZA KUKATWA KWA ABDUL NONDO KATIKA UCHAGUZI WA URAISI (DARUSO) 2017/2018.


Uchaguzi wa uraisi DARUSO mwaka 2017/2018.(Chuo kikuu cha DAR es Salaam ) Umekuwa na kelele nyingi kutoka kwa wanafunzi kutokana na wagombea waliopitishwa na wagombea waliowataka kukatwa kwa sababu ambazo, mimi Kama muandishi niliamua kuingia field kufanya uchunguzi kwa nini hayo, yalitokea.

Waliorudisha fomu walikuwa takribani 25 ,jambo ambalo walitakiwa chini ya 10,katika kufanya "sorting" .

Kwa taarifa za haraka haraka kulikuwa na kikundi cha ya wajumbe wa tume 7 Kati ya 13 ,ambao wenyewe walikuwa wanapokea maagizo nani apite nani asipiti, walianza tengeneza zengwe mwenyekiti wa conas na mwenyekiti wa coaf dhidi ya mgombea Matata wa cohu, kwa kumtuma mtu akasaini fomu ya udhamini, ndugu Matata aweke no ya mtu wa conas na mtu wa coaf, hapo wakasema mgombea huyo hana kigezo, sababu amedanganya.wakaweka a fomu pembeni.

Mgombea siti, pia hao hao wajumbe waliokuwa wanafanya Kazi kwa kupokea maagizo, walipokea maagizo siti asipiti, mwenyekiti wake wa COSS ndiye aliye husika kuchafua fomu ya ndugu siti, kwa kupitisha kalama juu, hivyo kuonekana hana sifa.



Kukatwa kwa Abdul Nondo., kukatwa kwa abduli Nondo sababu ni nyingi saana

1. Alihusishwa na itikadi ya chama kuwa ni mpinzani,

2. Alikataa kutoa rushwa ya laki 6,aliyoombwa na wajumbe fulani ili waampitishe.

3. Vijana wa Uvccm waliapa kupambana Abdul Nondo asipite,

4. wajumbe wa tume baadhi walipewa fedha ili kuhakikisha Abdul Nondo achomoki.

5. Utawala walipinga vikali sababu Abdul Nondo, alionekana harsh saana kipindi akitetea mikopo ya wanafunzi, hivyo hawataki kuona yaliyotokea yanatokea tena, hivyo waliagiza mtu huyo hatakiwi hata kidogo.

6. Utawala ulipinga vikali juu ya Nondo kupitishwa , sababu alipewa barua ya onyo alipo jiaribu kupeleka hoja bungeni kumuwajibisha Waziri mkuuu baada ya ufujaji wa fedha za shato (mabasi ya chuo) ,na mshauri wa wanafunzi aliingia na barua ya onyo aliyopewa Abdul Nondo, ili kuwakumbusha wajumbe kuwa mtu huyu utawala hawamtaki.

Haya ni maneno yalioongelewa na wajumbe wa tume tofauti tofauti wakisema interview Abdul Nondo alifanya vizuri ,hata hivyo angetakiwa kuondolewa mapema katika "sorting" ila waliona fujo na vurugu ingetokea Chuo, ofisi ya dean ilisema apitishwe akakatiwe katika screening, kweli wajumbe wakafanya hivyo, alisema mjumbe wa tume.


7.kuna watu maalumu waliopangwa na utawala kuwa ndio wanaotakiwa kupitishwa hivyo Abdul Nondo, alionekana ni msindikizaji katika ya wagombea 7,ambao walikuwa wakifanyiwa interview ili kupata watatu, ilikuwa ni lazima akatwe, na utawala wameapa kupambana nae asirudi DARUSO tena, hata kuteuliwa hatakiwi.



Hii imeonekana kuwa demokrasia ya DARUSO ni kuchukua fomu na kurudisha, wagombea wapo mfukoni na Hakuna uwezo wowote unaoangaliwa. Tume haipo huru inaingiliwa alisema mjumbe. 

Ni jambo la kushangaza wajumbe kumpa Abdul Nondo Zero ya mia, na hata leadership experience kupewa 0,Kana kwamba hajawahi kuwa kiongozi wakati alikuwa kaka mkuu kidato cha nne, kidato cha 6,pia Chuo amekuwa mbunge, Waziri pia, lakini walifumba macho wakaweka zero, walioweka mia ni wajumbe 6 tuu ila 7 wote waliweka 0.

No comments

Powered by Blogger.