-->

Header Ads

KANTE AWABURUZA HAZARD, IBRAHIMOVIC

Mara nyingi utamuona anatikisa kichwa, anatabasamu au anafanya tackles za maana dimbani. Hana maneno mengi, halalamiki hovyo, anafunga mara chache sana lakini shughuli yake timu pinzani inatambua.

Ni jamaa fulani mweusi hivi; mweusi tii, mfupi, hana makuu na pamoja na kulipwa mamilioni ya shilingi anaishi maisha ya kawaida sana.

Huyo ndiye N'golo Kante, kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya Chelsea ya Uingereza.) Kante "mkata umeme" ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa chama cha wanasoka wa kulipwa (Professional Footballers Association- PFA)

Tuzo za PFA hutolewa kwa mchezaji aliyefanya vizuri zaidi kwa msimu na kura zake hupigwa na wachezaji wenyewe. Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwa Kante baada ya kushinda ligi kuu huku hali ikionesha kuna uwezekano wa Kante kuvishwa tena medali ya ushindi wa ligi kuu akiwa na Chelsea ambayo hadi sasa iko kileleni kwa tofauti ya pointi nne na Tottenham inayofuatia katika nafasi ya pili. N'golo Kante ameshinda tuzo hiyo mbele ya mchezaji mwenzake wa Chelsea, Eden Hazard na akina Harry Kane, Zlatan Ibrahimovic, Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.
Katika usiku huo wa tuzo, mchezaji wa Tottenham Delle Alli aliibuka na tuzo ya mchezaji kinda, ikiwa mara yake ya pili mfululizo kushinda tuzo hiyo. Mchezaji wa zamani wa Manchester United, David Beckham alizawadiwa Merit Award kwa mchango wake kwenye soka.
 JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.