-->

Header Ads

JEURI; MORINHO AWAAMBIA DE GEA, ZLATAN NA WACHEZAJI WENGINE RUKSA KUONDOKA OLD TRAFFORD.


Gazeti moja maarufu la michezo la nchini Hispania linadai kocha wa Manchester United amewaambia baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wanaotaka kuondoka kwamba waondoke tu kama wanataka.

David De Gea, Ander Herrera na Zlatan Ibrahimovich ndio wachezaji waliotajwa na gazeti hilo kwamba wameambiwa na Mourinho baada ya kocha huyo kuchoshwa na tetesi kuhusu wachezaji hao.

David De Gea inaeleweka kwamba amekuwa akihusishwa na kurejea nchini kwao Hispania kuitumikia Real Madrid na kocha wake sasa anaonekana kuchoka kulizungumzia hilo na kuamua kama anaondoka baasi aondoke tu.

Ander Herrera naye pia inasemekana anataka kurudi nyumbani kwao Hispania kucheza soka, huku Zlatan akiwa haeleweki kwani hadi hivi sasa hajasaini mkataba mpya na mazungumzo yalikuwa yakiendelea hata kabla ya kupata majeruhi.

Nyota mwingine ambaye amekuwa akitajwa sana kwamba anaondoka Manchester United ni mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo ambaye ni Rooney tetesi zinasema huenda akafuata utajiri wa soka la China au Marekani.

Gazeti hilo la Marca linasema Mourinho amekuwa hataki utani kuhusu kukijenga kikosi kipya na anaamini katika nguvu aliyonayo kuleta wachezaji wapya na ndio maana akaamua kuweka wazi kwa wachezaji waliopo wanaotaka kuihama klabu hiyo.



TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU

No comments

Powered by Blogger.