TUMESAHAU
Mayowe
ya azimio, na mbiu nyingi angani
Tulipata
mafanikio,toka bara kule pwani
Tukafungua
sikio,nuru kuja hadharani
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
Jua
la utosi shamba, tulikunywa jasho letu
Tukajivika
kwa kamba, watupu mbele wanetu
wote
tukawa wembamba, wakanenepa wenzetu
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
Macho
hatukufumba,simanzi zikwisha katu
siamini
katu kwamba,jasho lile la meatu
Hata
la kule mkamba,leo huosha viatu
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
Hatuna
makimbilio,tunatapa tu vinywani
Vimetujaa
vilio, kusaka mchawi nani
Tulimwaga
visusio, ili tujitoe tunduni
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
Tumebaki
wa makisio,ya kesho za ndotoni
Iko
wapi mishikio,ilokamata garoni
Kwisha
tangu azimio,leo kauli vitani
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
Tumeyasahau
yale,tuliyo yapigania
Na
tulikotoka kule,tulianza moja nia
Wanavyosema
wale, walio tupigania
Tumesahau
tukotoka, mbuyu kama mchicha
No comments