-->

Header Ads

MSIBA: MZEE KIKWETE AONDOKEWA NA MAMA YAKE






Leo March 7 2017 zimeripotiwa taarifa za msiba kutoka kwenye familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete ambapo imeelezwa Nuru Kikwete ambaye ni mama mlezi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amefariki Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa. Rais mstaafu Kikwete kupitia account yake ya twitter ameandika haya kuhusu msiba huo.

"Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo kufuatia kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi. - JK"


"Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. - JK"


"Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo. - JK"


"Mama yetu mdogo aliitwa jana na Mola, na kuitika. Shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo. - JK"


"Mazishi yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri. - JK"


No comments

Powered by Blogger.