IMEFICHUKA: MSAMI KWENYE MAHUSIANO MAPYA NA CHEMICAL
MWANAMUZIKI aliyefahamika zaidi Bongo kupitia wimbo wake wa Mabawa, Msami Baby hivi karibuni amefunguka jinsi anavyomkubali msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Chemical jambo lililosababisha afanye juu chini ili kuweza kufanya kazi na mwanadada huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa.
Akichonga na Uwazi Showbiz, Msami alifunguka kuwa kwa muda mrefu alikuwa na ndoto za kufanya kazi na Chemical akaamua kuueleza uongozi wake uliofanya mazungumzo naye na kuweza kufanikisha kolabo ya wimbo wake mpya uitwao So Fine.
“Nimekuwa nikimpenda kwa muda mrefu Chemical hasa kufanya naye kazi, nakumbuka kabla ya hii kolabo hatukuwahi kuzungumza lolote zaidi ya salamu, hii kolabo imetuweka karibu zaidi,” alisema Msami.
LIVE KUTOKA TEGETA: Kituo cha Mafuta Chanusurika Kuteketea kwa Moto→
LIVE KUTOKA TEGETA: Kituo cha Mafuta Chanusurika Kuteketea kwa Moto→
No comments