HASIDI WA NCHI YENYE KUSADIKIKA
Machukio we chukiza, wakere walozubaa
Usijibane
kuwaza, weka kiza kwenye taa
Chukio lako
dubwaza, tema sumu kutambaa
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
Kamata
chini na kati, umalizie na juu
Kiziwi
hana shariti, nani wa kuvunja guu
Hana
kizazi thabiti, majuto si mjukuu
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
Mpanda
ngazi hushuka, hupanda bila tetema
Aghalabu
huanguka, wa mbele kurudi nyuma
Fyata
funga na funguka, hili jumba liko mrama
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
Uso mng’avu
hatari, na nywele zimepepea
Kwa
mafuta ya uturi, ni nngumu kuelezea
Kila
kukicha safari, hajui kwa kwelekea
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
Hata shauri
hataki, shupavu kama kidisa
Eti yeye ni
kisiki, hagawiki namba tasa
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
Tumtafute
shujaa, afanane na Daudi
Asiyewaka
tamaa, na kiu ya uhasidi
Yana katika
masaa, atatolewa kwa radi
Nalichukia
Hasidi, jabali mmeza haki
by Fulgence Makayula
No comments