-->

Header Ads

MWIGULU NCHEMBA ASEMA JAMBO


Wakati sakata la madawa ya kulevya likiendelea kuzungumziwa nchini, hatimaye waziri wa mambo ya ndani MWIGULU MCHEMBA ameibuka bungeni na kuyasema haya juu ya swala hilo la mihadarati

 ".......vita hii ya madawa ya kulevya ni ya kila mtanzania na vita hii haijaanza sasa, mimi tangia nilipofika nilikuta tayari Mh.Kitwanga ameshakamata mapapa wakubwa tu...na tulivyotoka pale tumeendeleza, na mimi niwaambie waheshimiwa wabunge ,tunaweza tukatofautiana kimtazamo kwenye approach na ninyi kama wabunge,kama washauri wetu mkitushauri njia nzuri ya kufikisha jamabo hili, sisi mara zote tutapokea ushauri huo kwa sababu vita hii si ya mtu mmoja ..........jambo moja tu ambalo nawaomba tuwe nalo, tusibadili lengo.....".

Swala la madawa ya kulevya limeshika kasi zaidi nchini na halikauki midomodi mwa watu kufuatia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwaita baadhi ya watu kufika  kituo kikuu cha polisi (central police station)  kwa mahojiano zaidi   wakiwemo wasanii na wafanya biashara wakubwa.

No comments

Powered by Blogger.