-->

Header Ads

MKUTANO KUHUSU LIBYA NCHINI MAREKANI wafutwa kutokana na amri ya Donald Trump

Mkutano kuhusu Libya uliokuwa umepangwa kufanyika nchini Marekani tarehe 16 mwezi huu umefutwa kutokana amri ya rais Donald Trump ya kupiga marufuku raia wa nchi saba za Kiislamu ikiwemo Libya kuingia nchini humo.
Mkutano huo uliokuwa ufanyike chini ya anuani ya "Uhusiano wa Marekani na Libya mwaka 2017; upeo mpya, matumaini na fursa" na unaosimamiwa na Baraza la Taifa la Uhusiano wa Libya na Marekani umeakhirishwa kufuatia amri hiyo ya Trump.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandalizi wa mkutano huo amri iliyotangazwa na rais wa Marekani itazuia kikamilifu hotuba zote, wafadhili na wageni walioalikwa katika mkutano huo uliopangwa kufanyika mjini Washington. 
Ajenda kuu ya mkutano huo ni nafasi ya sekta ya mafuta katika uthabiti wa uchumi na umuhimu wa uthabiti wa uchumi kwa uthabiti wa kisiasa.
Mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Libya pamoja na Mkuu wa Shirika la Taifa la Mafuta la nchi hiyo ni miongoni mwa watu waliotazamiwa kushiriki kwenye mkutano huo.
Imeelezwa kuwa mkutano huo umeakhirishwa na tarehe ya kufanyika kwake bado haijajulikana.

No comments

Powered by Blogger.