-->

Header Ads

RAIS wa zamani wa TUNISIA AHUKUMIWA KIFUNGO JELA LICHA YA KUTOKUWEPO MAHAKAMANI


Dikteta aliyeondolewa madarakani wa Tunisia amehukumiwa kifungo cha miaka 8 jela bila ya kuwepo mahakamani.
Mahakama ya Tunisia imemhukumu Zainul Abidin bin Ali kifungo cha miaka 8 jela katika kikao kilichofanyika jana Ijumaa bila ya dikteta huyo kuwepo mahakamani.
Mahakama hiyo pia imemhukumu mkwe wa Zainul Abidin aliyekimbilia katika kisiwa cha Ushelisheli kifungo cha miaka 6 jela.
Rais wa zamani wa Tunisia ambaye tayari amehukumiwa vifungo mara kadhaa tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2011, mara hii amehukumiwa kifungo kwa kupatikana na hatia ya kutumia vibaya vyombo vya dola kwa maslahi yake binafsi. Zainul Abidin na mkwewe pia wamehukumiwa kulipa faini ya Euro laki nne. 

Awali mahakama ya Tunisia ilimhukumu Zainul Abidin kifungo cha maisha jela kutokana na mauaji ya raia 338 wakati wa harakati ya mapinduzi ya wananchi mwaka 2011. Dikteta huyo wa zamani wa Tunisia amekimbilia Saudi Arabia anakopewa hifadhi na utawala wa kifalme wa nchi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.