-->

Header Ads

Rais Kiir kwa mara nyingine ataka kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara nyingine, ametoa wito kwa wanasiasa na makundi ya waasi nchini humo kukubali kuweka silaha chini ili kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa.



Kiir amewaambia wabunge jijini Juba kuwa njia pekee ya kumaliza tofauti za kisiasa, vita na baa la njaa linalowasumbua raia wa nchi hiyo, ni kuja pamoja na kuzungumza.
Mwezi Desemba mwaka 2016, kiongozi huyo wa taifa changa zaidi duniani, alitangaza umuhimu wa mazungumzo hayo ili kumaliza mzozo wa zaidi ya miaka mitatu nchini humo.
Mwaka 2015, kiongozi huyo na kiongozi wa sasa wa waasi Riek Machar ambaye alikuwa Makamu wake wa rais, walitia saini mkataba wa kusitisha vita na kuunda serikali ya mpito lakini mkataba huo ulivunjika mwaka uliopita.
Serikali na upinzani wamekuwa wakilaumiana kuhusu kuvunjika kwa mkataba huo ambao umesababisha kuendelea kwa vita nchini humo na kusababisha Machar na wafuasi wake kuishi nje ya nchi hiyo.
Wito huu rais Kiir umekuja wakati huu, Umoja wa Mataifa ukisema nusu ya raia wa nchi hiyo wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na vita vinavyondelea kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.
Melfu ya watu wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao.
 

No comments

Powered by Blogger.