BREAKING: MTANDAO WA WANAFUNZI WAUNGANA NA LHRC KUPINGA MALIPO YA 15% YA BODI YA MIKOPO
Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) kupitia kurugenzi yetu ya sheria, kama wahanga watarajiwa, tumeafikiana na mawakili wetu takribani 10, kuungana na mawakili wa kituo cha haki na sheria (LHRC) kwajili ya kwenda mahakamani kupinga malipo ya 15% kwa bodi ya mikopo ambayo awali yalikuwa ni 8%.
TSNP tunatoa wito kwa chama cha walimu Tanzania (CWT), Muungano wa wafanyakazi katika sekta ya viwanda na biashara (TUICO), Umoja wa wafanyakazi wa afya wa serikali (TUGHE), Muungano wa wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) na wadau wengine wenye maslahi na suala hili, kujitokeza na kuunganisha nguvu zetu kwajili ya kupinga ongezeko hili la 15% (zaidi ya 80%) katika vyombo vya sheria.
Tunawapongeza sana LHRC kwa jambo hili muhimu. kikao cha kuleta muafaka kitaketi kesho kutwa ya juma nne ya tarehe 28, kwenye ofisi za LHRC.
IMETOLEWA NA ©Bob Wangwe
-Mkurugenzi wa sheria TSNP
-Mkurugenzi wa sheria TSNP
No comments