-->

Header Ads

Ujenzi wa wodi mpya katika hospitali ya MAWENZI waepusha magonjwa ya mlipuko kwa watoto.

Watoto wanaolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa KILIMANJARO MAWENZI wameondokana na tatizo la kupata magonjwa ya milipuko kutokana na msongamano waliokuwa nao katika jengo la kulazia watoto

mmoja wa akina mama akimuuguza mwanae akiwa wodini

Watoto wanaolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa KILIMANJARO MAWENZI wameondokana na tatizo la kupata magonjwa ya milipuko kutokana na msongamano waliokuwa nao katika jengo la kulazia watoto la hapo awali baada ya kukarabatiwa kwa wodi nyingine ya watoto.

Mkuu wa idara ya watoto hospitali ya MAWENZI, Dkt WINFRIDA SHOO amesema kuwa kukarabaitiwa kwa jengo hilo kutasaidia kuondoa msongamano kwa watoto wanaolazwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO, SAID MECK SADICK amesema baadhi ya majengo ya hospitali hiyo ni chakavu na yanahitaji kufanyiwa ukarabati na serikali kwa  kushirikiana na wadau mbalimbali

No comments

Powered by Blogger.