Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE yafanikisha upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 6 bila kutumia mashine.
Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE iliyopo Jijini Dar es salaam ikishirikiana na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya APOLLO ya nchini INDIA imefanikiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo sita bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.
Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE – JKCI iliyopo Jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya APOLLO ya nchini INDIA imefanikiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo Sita bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, mmoja wa madakta wa taasisi hiyo Dkt. BASHARI NYANGASA amesema kuwa upasuaji huo umesahidia kupunguza madhara ambayo yangetokana na kutumia mashine hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tiba ya moyo Dkt. PETER KISENGE amesema kuwa upasuaji wa aina hiyo ni ni endelevu na kutoa wito kwa madaktari wote nchini kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo ya moyo katika taasisi hiyo ili wakapatiwe matibabu.
Upasuaji huo kwa wagonjwa wa moyo SITA ndani ya nchi umeisaidia serikali kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 170 ambazo zingetumika endapo wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi.
No comments