-->

Header Ads

Serikali Tanzania Kutoa Ajira Mpya1500 kwa Jeshi la Polisi

Rais Magufuli ameridhia ombi la IGP Sirro la kuajiri askari 1500 ili kuongeza nguvu katika jeshi hilo.
“IGP Siro ameniambia kwamba anahitaji kuongeza idadi ya polisi, sasa ninakuruhusu kuajiri watu 1500 ili wawe pilisi. Hakikisha hamuajiri ndugu zenu…waajirini Watanzania…watoto wa masikini,” alisema wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na Wafanyabiashara Mkoani Arusha.
Nyumba hizi zimejengwa baada ya zilizokuwepo kuungua moto mwaka jana.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameridhia kupandishwa kwa vyeo kwa baadhi ya askari ambao walistahili.
“Hawa maafisa mnaotaka wapandishwe vyeo, kaa na maafisa wenzako mlete mapendekezo..mimi nitawapandisha. Pasiwepo upendeleo,” alisema Rais Magufuli huku akisisitiza kwamba, “ninataka mtembee kifua mbele, maneno ya kashfa na kebehi mnayopewa na watu wachache yasiwakatishe tamaa. Mimi niko pamoja nayi…sita waacha,”

No comments

Powered by Blogger.