-->

Header Ads

SERIKALI YATUPIA JICHO SEKTA YA UVUVI NCHINI

Serikali  imesema inampango mkakati mzuri katika kuendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi na kutoa ajira za uhakika kwa Watanzania ambao wanafanya shughuli hiyo.

Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amesma hayo akiwa Soko la Samaki Msasani wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi kwa wavuvi waliofanya vizuri katika mashindano yakuvua samaki kwa vitumbwi na ngalawa yalioandaliwa na taasisi ya Tuna ambapo mshindi wa kwanza alipata tsh 400,000, wapili tsh 300,000 na wa tatu tsh 200,000.

Alisema serikali  imesema  inampango na mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi ili sekta hiyo iweze kufanya vizuri na kusonga mbele zaidi

Meya alisema wavuvi  wanapaswa kuwa wabunifu ili kusaidia sekta hiyo kufanya vizuri zaidi

Afisa Uvuvi wa Manispaa Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza katika kilele hicho amesema kama kuwa watahakikisha wavuvi wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili waweze kuinuka kwa kipato zaidi.


KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu

No comments

Powered by Blogger.