Gwajima amuamshia 'Dude' Nyalandu

Siku
kadhaa aada ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samwel
Nyalandu kutangaza kukihama Chama Cha CCM kwa madai kimepoteza mwelekeo
na kushindwa kuikosoa serikali, Kada wa chama hicho aitwaye Methusela
Gwajima, amemjibu mwanasiasa huyo kwa kumwambia sababu alizotoa ni za
kitoto sambamba na kueleza baadhi ya mafanikio na mambo ambayo
yamefanywa na serikali hiyo inayoongozwa na chama cha CCM.
Hata
hivyo kada huyo ameweka wazi kuwa huenda kilichomuondoa Nyalandu ni
baada ya kusikia kuwa anachunguzwa tuhuma za mambo aliyofanya akiwa
Waziri wa mali asili na utalii na kwamba ameshindwa kusubiri kuumbuliwa
kwakuwa yalikiaibisha Chama cha mapinduzi na kuitia Nchi hasara.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments