Emmerson Mnangagwa Kuapishwa Kuwa Rais wa zimbabwe Ijumaa Hii
Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa, limesema shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC)
Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.
Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.
Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane
Katika barua hiyo , Bwana Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu ukabidhianaji wa mamlaka wa amani, na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments