AVEVA NA KABURU wa Simba Waendelea Kusota
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya utakatishaji fedha
na kugushi inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ hadi October 11, 2017 kwa sababu upelelezi
haujakamilika.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine ambapo baada ya kueleza hayo Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017.
Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.
Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,