Nilitegemea Hili Kutokea- Zitto Kabwe

Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina
pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa jana na kampuni ya
Barrick Gold Mining, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na
kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.
Mh. Kabwe amesema alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi.
Mh. Zitto amesema kwamba tangu jana alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.
"Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.

KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments