KISIWA CHA ZUNIGA (6)
Na Adalgisa Kweka.
Ilimuwia vigumu kwa Tuli kuamini kuwa Victor amekufa wakati bado hawakutimiza adhimio lao lakutoroka kisiwani hapo licha yakwamba hakukuwa na historia ya watu kutoroka kisiwani hapo ndomana hata wazazi wao hawakujua chochote.
"ha-pa-na si Victor"kauli hii ilimfanya Tuli afarijike kidogo.
"ni rafiki yangu nimemjua Jana tu Tu-li leo-(alianza kulia huku kwikwi ya kilio ikiuumiza moyo mdogo) Tuli LAZIMA TUONDOKE KWENYE HIKI KISIWA LAZIMA"saluat alibadilika ghafla nikama pepo lilimnyemelea nakumvaa ghafla kiasi chakumfanya asahau huzuni yake na kifo cha koku, kibaya zaidi alishasahau wapo na mzawa chumbani hapo. Tuli alimfinya rafiki yake huyo iliazinduke nakurejesha akili zake kwenye wakati uliopo na siujao walauliopita lakini haikusaidia.
"Tuli, Joe amekufa,koku amekufa na sisi tukombioni kufa if we won't do anything (kama hatutofanya chochote" huyu hakuwa yule saluat aliyekutana naye.
"salu!!" alimuita aliona rafiki yake alikuwa anakigongea kifo, alimsogelea nakumng'oneza "Kuna mzawa salu shshh". Ghafla akili zilimzinduka alimuangalia mzawa yule ambaye alikuwa kimya masaa yote utafikiri alikuwa mwenyeji mwenzao.macho yao yalikutana,mapigo ya moyo yalimuenda mbio sana hakuwa nachakusema Zaidi yakubaki anamuangalia tu kwani macho yake yalichukua nafasi ya mdomo yaliongea mengi tu. Tuli alikuwa amemshikilia rafiki yake huyo huku ukimya ukitawala ndani ya chumba hicho ghafla,zimwi la kifo lilivamia chumba hicho bila kukaribishwa. Wakiwa bado kimya kila mtu asijue chakufanya mlango wa chumba hicho ulifunguliwa ndipo mzawa mwingine alipoingia, hapo akina saluat waliweka roho zao mkononi walishahisi yule mzawa aliyasikia mazungumzo yao yote ndomana alifika chumbani hapo tena bila hodi!!
"mzawa!"alimuita mzawa mwenzie ambaye alikuwa na akina saluat.
"Ndyo mzawa" aliitikia.
"Kuna tatizo gani hapa"aliuliza mzawa yule swali lake liliwafanya akina saluat wajue kuwa yule mzawa hakusikia chochote hivyo hakujua kilichoendelea hapo hofu yao ilikuja kwa huyo mzawa waliyekuwa naye ambaye alisikia kila kitu, kwenye fikra zao walimlaumu pepo aliyempitia saluat.
"Kuna huyu mwenyeji amezidiwa kidogo ndo nimemleta hapa" hatimaye aliongea maneno ambayo hawakuyategemea,kwa salu alibaki vilevile kama mzawa Malaika lakini kwa Tuli huyu alikuwa Mzawa WA ajabu kuliko hata yule alyemziba macho siku ile usiku.
"aaah nimepewa taarifa na mzawa pale mapokezi"
"Ndyo alituambia tumlete hapa"
"Sawa mzawa unaenza kwenda, Tuli kaendelee na kazi yako"ilikuwa ni rahisi kumjua Tuli ni nani katakana na jinsi saluat aliyokaa kinyonge huku macho yake Yakiwa mekundu mithili ya moto WA Jehanamu.
Tuli na yule mzawa malaika waliondoka mule chumbani, ila koo la tuli lilimuwashawasha kama fungus kwenye miguu alijikuta akimshukuru mzawa yule bila kujua kua hamnaga kitu kinachofanywa bure kila kitu kinamalipo yake.
"Asante Sana mzawa"shukrani yake ilitoka kwenye chembechembe za moyo wake nakusafirishwa kwa damu hadi kufikia kutoka kinywani mwake hadi yule mzawa alilijua hilo.
"KAENDELEE NA KAZI"hakuitikia shukrani baadala yake alivaa sura ya uzawa kabisa alihisi ubinadamu unampitia Sana. Tuli alimsindikiza kwa macho mzawa yule bila kuamini kama ni kweli alikuwa mzawa au mwenyeji.
"mzawa" ilikuwa sauti ya mjamzito,tuli aliangalia huku na huku hakumuona mzawa yeyote zaidi ya yeye mwenyewe. Alijua kuwa yeye ndo alikuwa anaitwa alimsogelea kijana mwenzie huyo kuonyesha ameitikia wito.
"kichw-a kinauma" alimwambia Saluat kwa huzuni sana kuonyesha kuwa maumivu yalimtesa kweli na siutani.
"usihofu jikaze nikafuate dawa" alimpa moyo mjamzito huyo. Tuli aliangalia pembeni aliona makaratasi yaliyokuwa na nembo ya hospitali, tuli aliyashika nakuanza kuyasoma,alipomaliza aliyaweka chini nakuangaza macho huku na kule ndipo alipoona kabati lenye dawa, alianza kutembea lilipo kabati alifikanakulifungua Kisha kutafuta dawa ambayo aliihitaji alipoipata,aliichukua Kisha kufunga kabati nakurejea kwa yule mjamzito ambapo alimkuta akiendelea kuyalalamikia maumivu ya kichwa.alimsaidia kutoa vidonge Kisha akampa ameze.
"meza maumivu yatupungua taratibu" alimsisitizia kutokana na ujuzi wake katika suala la unesi, kabla yakufika kisiwani hapo alikuwa katika mafunzo ya vitendo almaarufu kama field katika hospitali ya mnazi moja katika wodi ya wazazi hvyo alijua.
"usi-ni-u-e"aliongea kwa huzuni, maneno yaliyomtoka aliyamaanisha kabisa. Tuli alishtushwa na maneno moja kwa moja akajua kwamba mjamzito yule alihisi amempa dawa zakumuua na sikumponya na maumivu ya kichwa.
"mimi si mzawa, nipo kwenye kitengo" alimtoa hofu yule mjamzito ambaye baada yakusikia maneno Yale alimeza zile dawa Kisha akamshukuru.
"Nesi"mjamzito mwingine alimuita huyu alimuita kitofauti kidogo nakumfanya ajihisi yuko duniani, tena kwenye hospitali Kubwa akiwa kama Nesi wa zamu ijapokuwa haikuwa kweli chozi lilimtoka ni chozi lililokuwa na mang'uniko mengi juu ya maisha yake, alilifuta chozi lile nakwenda kumsikiliza mgonjwa yule.
"Nesi nimechoka"ilikuwa ni kauli ya yule mjamzito ni kauli iliyompa maswali juu ya nini hasa kilichomchosha? Na kama amechoka alihitaji nini hasa?
"pole Sana" alichukua makaratasi yake nakuyapitia, aligundua kuwa alikuwa anatarajia mapacha tena wajinsia ya kiume ila kikubwa zaidi alikuwa anatarajia kujifungua siku zakaribuni.
"haisaidii" alimjibu Tuli ambaye alikuwa anayapitia makaratasi yake.
"vumilia utajifungua siku zijazo"alimpa moyo
"sitaki kuji-fungua"aliweka wazi nia yake, nia iliyomshtua Tuli mwenyewe.
"kwanini wakati Muda unakarbia"alihitaji kujua sababu hakuona sababu yakukaa na mimba miezi yote nane alafu WA tisa umeingia akatae kuzaa.
"kwanini?wewe hujui?" alimgeuzia kibao Tuli ambaye alibaki anamshangaa tu kijana mwenzie ambaye ni mama WA watoto wawili mtarajiwa.
"mimi ni mgeni hapa ntajuaje"alianza kukikana cheo chake cha uenyeji alichopewa na kisiwa hiko, alihitaji kujua sababu na sikingine.
"wewe ungependa uzae ndani ya kisiwa? Ungependa mtoto wako akue ndani ya hiki kisiwa? Ungependa ufe umuache mtoto wako kwenye hiki kisi-wa?"alikuwa analia, maneno yake yalikuwa kama mkuki WA moto kwenye moyo wake, yyaliuchoma vilivyo alianza kukumbuka matukio yote tangu anachukuliwa kwao mpaka siku hiyo alipata jibu zuri, hakukuwa na kitu kizuri kwenye hiko kisiwa ambacho mtoto wake angependa akione zaidi ya majengo mazuri na ya gharama.
"nauliza ungependa!!? (Tuli hakumjibu,)ungependa mwanao awe MZAWA?" hapo alimshtua Tuli tena sana.
"MZAWA!!?"alionyesha kila hali yakushtushwa hakuelewa watoto wakizaliwa wanapelekwa wapi na wanalelewa na nani.
"ndyo" alimshika mkono Tuli nakumsogeza karibu yake nakuanza kumng'oneza "mtoto akizaliwa analelewa ili awe mzawa wa baadaye ndomama wanataka watoto wakiume,ukizaa wakike adhabu yake ni kifo wote wawili na ukizaa wakiume usipokuwa mzma wa afya kifo kitakuandama vilevile ndiomaana nahitaji Masada wako" maneno ya yule mjamzito yalimshtua sana alikuwa na maswali mengi sana ambayo muda haukumtosha kumuuliza yote.
"siwezi shiriki dhambi hii"aliweka wazi dhamira yake hakutaka kuwa muuaji hata kidogo.
"Bali unataka kushiriki dhambi yakuwaacha malaika hawa waje waishi maisha yakuwa wakatili!!"mjamzito yule aliweza kucheza na akili ya Tuli vizuri kiasi chakumuacha njia panda asijue dhambi ni ipi.
"sitaki wanangu waje wamwage damu, sitaki waje waishi kwenye hiki kisiwa nataka nife nao hii dhambi ntakufa nayo mwenyewe naomba unisaidie dawa tu hata sindano" hii ilimtisha yaani mtu alikuwa akiiomba kufa ili awaepushie balaa watoto wake.
"what if Kuna Kamera zinaturekodi?" Hilo lilikuwa swali la msingi hakufikiri wazawa ni wajinga kiasi hiko kwamba wasifunge Kamera za kuchukua matukio yanayoendelea humo ndani walijua haya yanaweza tokea na yeye hakutaka kuwa kwenye wakati mgumu na wamiliki wa kisiwa wala kuiharibu mipango yake kwani tiyari alishahiharibu.
"ndomana nimekunong'oneza ili ionekana mm nakuongelesha ila wewe ukiinuka unajifanya unakataa" mjamzito alikuwa amedhamiria kuuondoa uhai wake na wawatoto wake hata Tuli alianza kuelewa dhamira yake.
"kama huwezi kuniletea nionyeshe wapi pakuzipata dawa hizo au nitajie majina yake mimi nitazichukua usiku ili kukuepushia matatizo" Tuli hakuweza kukataa tena alimtajia dawa mbili alizozijua"endapo daktari atamuandikia mjamzito dawa hizi Atakuwa anamuua taratibu inachukua siku nne tu anakufa"alikumbuka maneno ya mhadhiri wake. Alimtajia majina ya hizo dawa na muda wakuzitumia pamoja na dalili atazozisikia.
"HAPANA HAIWEZEKANI!! Hilo sijambo ZURI, SIWEZI SHIRIKI KABISA!!" tuli alishaiuachia mkono WA mjamzito yule nakuanza igizo lake kama alivyoelekezwa,alipomaliza alirudi kule chumbani kwake ambapo alimkuta saluat akiwa amelazwa kitandani huku akiwa amewekewa kitambaa kilicholoweshwa na maji kichwani.
"Kazi imeisha!!" aliuliza mzawa Jose
"Ndio mzawa"aliitikia kwa ukakamavu bila kusita hakutaka kutengeneza mazingira yakuhisiwa chochote. Alimuelezea alichowapa huku akimwambia Kuwa mjamzito wa pili alimsumbua sana,alijua kwakusema hivyo kungemsaidia baadaye.
"Sawa, sasa kaa na huyu mgonjwa kwa Leo ila kesho atarudi anapostahili Kuwa"akimwambia Tuli ila mzawa huyo hakuwa Sawa hali hiyo ilijidhihirisha kutokana na uongeaji wake, Tuli alijua chanzo ni yale yaliyotokea Jana.
"Sawa Mzawa"aliitikia. Mzawa Jose aliondoka nakumuacha Tuli na rafiki yake saluat laiti angelijua juu ya urafiki wao asingekubali saluat alale kwenye kile chumba.
"pole" tuli alimwambia Saluat ambaye alionekana Kuwa na nafuu kidogo.
"Asante ulifikaje kwenye hiki kitengo" hili lilikuwa swali la muhimu kwanza kwani walikubaliana kuchagua kilimo.
"mmh nilichagua kilimo lakini yule mzawa alinipeleka Afya chaajabu zaidi huyu ndiye yule mzawa aliyeniziba macho usiku WA kwanza pale kisiwani" saluat hakuelewa chochote "siku wahi kukwambia kumbee--"Tuli alilishtukia hilo alianza kumuelezea kisa chote saluat alielewa vizuri.
"duu! Hiyo ni Neema" alimwambia Tuli kwani yule mzawa alikuwa na uwezo wakuitoa roho yake usiku ule. Saluat akamuelezea Tuli kuhusu koku na mzawa yule waliyekuwa naye mchana ule, stori ya Koku ilimtia huruma sana, saluat alijitahidi asilie akiwa anaelezea lakini ilipofika sehemu ya kunyongwa kwa koku akili ilimrudisha kwenye ule mwili aliouona kwa mbali ukining'inia alianza kulia.
"polee Salu"alimbembeleza rafiki yake huyo
"hapa natafakari kurudi kwenye kile chumba naogopa sana ile picha yake ya mwisho imegoma kufutika kichwani mwangu"
"pole sana.. Tumepiga stori mpaka giza limeingia hata hatujaenda kula" alivyoziita stori utafikiri zilikuwa stori kweli, zilikuwa ni simulizi za kweli zilizotisha.
"duu kweli" alichungulia nje nakuona giza
"watu walisharudi ngoja nkachukue chakula nkuletee na wewe" aliinuka na kwenda kufungua mlango,alipofungua alikutana uso kwa uso na yule mama WA mapokezi akiwa amebeba chakula cha watu wawili, Tuli alimpokea Kisha kuufunga mlango.
"kaa mkao wa kula" alimwambia Salu walifanya kama wako nyumbani. Salu aliinuka nakuanza kula.
"kazi zikoje?" aliuliza saluat swali lililomfanya Tuli akumbuke aliyoyasahau kumwambia kuhusu kazi yake. Tuli alianza kumuelezea kisa kipya kilichosisimua zaidi.
"mmh Kisiwa kina maajabu hiki Mungu atusaidie" alisema saluat
"yaani kila siku najua siri mpya ya Kisiwa na hofu sijui kesho ntajua nini"
"eeh Tutapona kweli??" aliuliza saluat swali ambalo hakuna aliyejua jibu Lake. Muda ulienda hatimaye walimaliza kula nakutoa vyombo nje Kisha kurudi Ndani ili walale. Usingizi uliwavamia nakuwachukua kimyakimya kuwapeleka ulimwengu mwingine.
*________*______________*_______________*______*
"Nini hikoo!!"Tuli alishtuka usingizini baada yakusikia makelele ya mlango kupigwa kwa nguvu. Alipoangalia mlangoni aliuona mlango ukiwa huku watu wanne wakimuangalia aliweza kumtambua mmoja ambaye ni Mzawa Jose ila wengine sura zilikuwa ngeni, hakujua ujio wao ulikuwa wa nini tena usiku huo, Tuli alikuwa anawaangalia kana kwamba anawasubiri wajieleze nini kilichowasibu mpaka wamvamie usiku huo.
"MKAMATENI!!" amri ilitoka kwenye kinywa cha Mzawa Jose, Tuli bado hakuelewa kinachoendelea walimkamata kwa lipi hasa.
"nimefanya kosa gani?" aliuliza Tuli ila hakujibiwa, hakuna aliyemjibu Bali walimvuta nakutii amri. Walimtoa chumbani kwake waliendelea kumvuta walipokaribia maeneo ya vitanda vya wajawazito vyenye watu Tuli, aliona damu pale chini hakutaka kuamini aliporudisha macho yake pale kitandani alikutana na sura ya mjamzito yule ikimuangalia alikuwa hajakata roho bado ila alitilia huruma damu zilitapakaa kitandani pake hakikua kifo kizuri. "itachukua siku nne mpaka kufa"alikumbuka maneno ya mhadhiri wa chuo."amekufa.." alijisemea Tuli kimoyomoyo. Alimuangalia yule mjamzito tena, raundi hii aliachia tabasamu jembamba lililomuumiza Tuli.
"sipumui" aliongea Tuli, lakini hawakumsikiliza
"Msimsikilize muuaji" alishakuwa muuaji tiyari mara hii.
"Dear God I DIDN'T KILL HER!..(Ee Mungu sijamuua")alisema kimoyomoyo ghafla nguvu zilimuishia, aliona giza mbele yake licha ya macho yake Kuwa wazi, mwili wake ulimlegea papohapo alipoteza fahamu akiwa mikononi mwa washurutishaji.........ITAENDELEA...