-->

Header Ads

Vikao vya uongozi vya Taifa vya Chama cha Mapinduzi (CCM), KESHO


 vinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey  Polepole leo Jumapili imesema vikao hivyo vya Taifa ni kwa mujibu wa ratiba ya kawaida.
Amesema pamoja na mambo mengine, vitakuwa na kazi ya kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wana CCM ambao wameomba dhamana ya uongozi katika ngazi ya wilaya.
Taarifa hiyo imesema Kamati Kuu itakaa Septemba 27 na 28 na  Halmashauri Kuu ya Taifa itakaa Septemba 30 hadi Oktoba Mosi jijini Dar es Salaam.



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.