VIDEO-Rais Museveni aagiza uchunguzi ajali iliyoua Watanzania 13
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema upelelezi kubaini sababu
za ajali iliyosababisha vifo vya Watanzania 13 waliokuwa wakitoka
harusini nchini humo unaendelea.
Waziri wa Ofisi ya
Rais anayeshughulikia Jiji la Kampala, Bety Kamya akisoma salamu za
rambirambi kutoka kwa Rais Museveni amesema licha ya kutoa pole kwa
familia, kiongozi huyo ameagiza uchunguzi wa sababu za ajali ufanyike.
Amesema pia amewapongeza maharusi, Dk Aneth na Dk Trease Ibingira na amewatakiwa maisha mema ya ndoa.
Mbali ya hilo, amesema anawaombea ili kukabiliana na kipindi kigumu walichonacho.
Amesema Rais anawashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu cha kupoteza wapendwa wao.
"Nakabidhi
vyeti hivi vya vifo vya ndugu zetu 13 nawapa pole sana," amesema Waziri
Kamya akimkabidhi vyeti hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora, Angellah Kairuki.
Waziri Kairuki amesema
Rais John Magufuli amepokea taarifa ya vifo hivyo kwa mshtuko na alitoa
maelekezo ya kupokewa miili hiyo, kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi
Lugalo, kuagiwa hapo na kusafirishwa kwa maziko.
Amesema maagizo hayo wanaendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa magari kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo.
Waziri Kairuki amesema kwa namna isiyo katika wakati wa kawaida, anawapongeza maharusi na kuwatakia maisha mema.
"Haya ni mapenzi ya Mungu, hili lisiwanyong'onyeshe maharusi," amesema Kairuki.
Ameishukuru Serikali ya Uganda kwa kukodi ndege kuirudisha nyumbani miili hiyo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments