Kwa maneno haya Zari kamaanisha nini?

Baada ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kukiri kuzaa mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto, hatimaye
mama watoto wake Zari Hassan ‘Zari’ azidi kumuweka njia panda msanii
huyo juu ya uhusiano wao.
Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kupokea
ushauri uliotolewa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.
“Watu wakiamua kuchepuka au kudanganya ni sawa na kujipotezea muda,
ingawa wanahisi wanakuchezea wewe, hivyo usikate tamaa na usijilaumu kwa
ajili ya makosa ya wengine, maisha lazima yaendelee,”
“Mambo yaliyotokea hayawezi kunipunguzia hadhi yangu, usijilaumu kwa
yaliyotokea, zingatia malengo yako na kufanya maisha yaendelee,”
amesema.
Amesema kuwa yale yote yaliyosemwa katika sakata hili yanabaki yalivyo
na muda huu anaamua kuyaweka kando na kuelekeza nguvu zake kwenye
maandalizi ya sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Sakata hili limeibuka siku moja baada ya Zari kujibu mapigo katika
mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe na kitendo alichokifanya Diamond
cha kuzaa na Mobeto.
Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na
mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba
ameelewa na hakuna tatizo tena.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments