Tafrani yazuka Bomoa Bomoa, Hivi ndivyo Wananchi wa Jangwani walivyopambana na Polisi leo
Wakazi wa Jangwani jijini Dar es Salaam, leo wamepambana na polisi na kusababisha vurugu katika barabara ya Morogoro.
Wananchi hao walikuwa wakizuia tingatinga la bomoa bomoa lisibomoe
nyumba zao zilizoko bondeni kwa kuwarushia mawe hatua iliyowalazimu
kutoa taarifa polisi ambao walikuja baada ya muda mfupi na kuwatawanya
kwa kufyatua risasi na mabomu ya machozi huku wananchi hao akiwarushia
mawe polisi hao.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wananchi hao
wamedhibitiwa na zoezi la ubomoaji linaendelea.
Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments