AFYA YA MBUNGE SAED KUBENEA YAKWAMISHA KAMATI YA BUNGE KUMUHOJI LEO..
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es salam (Chadema), Saed Kubenea leo alilazimika kupelekwa katika zahanati ya Bunge baada ya afya yake kutokuwa sawa.
Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Jumatano kuwa,
Kubenea amefika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na
amewaeleza kwamba hali yake si nzuri.
Kutokana na hilo, amesema amepelekwa kwenye zahanati hiyo na hali yake itakapoimarika atahojiwa na kamati.
Mbunge huyo ambaye alipelekwa Dodoma kwa ndege leo asubuhi, jana Jumanne
alisema alikuwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni
akisubiri utaratibu wa safari hiyo ya kwenda kuhojiwa kama Spika wa
Bunge Job Ndugai alivyoagiza.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments