Povu la H Baba kwa Diamond baada ya kutajwa kwenye 'zilipendwa'
STAA wa muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na ngoma zake kama Mpenzi Bubu, Kula Lazima na Nipe Kidogo, Hamis Baba ‘H Baba’, ameibuka na kujibu ‘Shit’ za mwanamuziki aliyemdiss kupitia ngoma yake, kwa kusema kwamba H Baba ni jina kubwa, hivyo hawezi kutafuta kiki kupitia yeye, na kuongeza kwamba msanii mwenyewe ni mwizi.
H Baba ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha TV na kusema:
“Kama kweli anatumia akili yake kufanya kazi, ataendelea kufanya kazi, lakini kama anajijua ni mwizi basi ajue mwisho wake umefika kwa sababu kazi za wizi siyo nzuri, bora angeiba nje, wangapi wanaiba nje? Unamuibia Mtanzania mwenziyo na ni mwanamuziki mwenziyo.
“Halafu unawaambia watu eti anatafuta jina huyo, mimi nitafute jina kupitia wewe, umetoka juzi tu jina lenyewe hilo ni dhahabu kwetu sisi, lakini H baba ni jina kubwa, ukigugo tu kwenye Internet H Baba linakuja.
“Ila ukitafuta jina lako unalitafuta kwa shida, jina langu ni kubwa sana kuliko wewe, utasubiri sana, kazi za wizi ndiyo mwisho wake,”.
H Baba ametoa povu hilo baada ya mwanamuziki flani wa Bongo Fleva, kumuimba kuwa amefulia kimuziki.

No comments