Nchi 134 zaunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran
Nchi za Kundi la 77 (G77) zimetoa taarifa na
kutangaza kuunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama
Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji, JCPOA huku zikisisitiza ulazima
wa kuondolewa vikwazo vyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo yamebainika katika taarifa iliyotolewa na mawaziri wa
mambo ya nje wa nchi wanachama wa G77 pembizoni mwa kikao cha Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa mjini New York. Katika taarifa yao, mawaziri wa
mambo ya nje wa G77 wamesema JCPOA ni mapatano yanayopaswa kuigwa na ni
mfano wa utendaji kazi wenye mafanikio wa mfumo wa pande kadhaa wa
kimataifa katika utatuzi wa masuala muhimu ya dunia.Mawaziri hao wa mashauri ya kigeni kutoka nchi 134 katika taarifa yao pia wamesisitiza ulazima wa kuondolewa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kikao cha mawaziri wa mashauri ya kigeni wa G77 kimefanyika Ijumaa na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo Ghulamali Khoshroo, Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema baada ya hotuba dhidi ya Iran na iliyojaa utata ya Rais Trump wa Marekani katika Baraza Kuu la umoja huo siku ya Jumanne kwamba nchi za G77 zimetangaza kuunga mkono kikamilifu mapatano ya nyuklia ya Iran na kutaka nchi hii iondolewe vikwazo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments