Mongella: Akijua Magufuli kuna Mtu atapona hapa?
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amefunguka na kuonyesha kusikitishwa na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambao wameshindwa kutumia gari ya kubeba wagonjwa jambo ambalo anasema kama Rais Magufuli angejua angewaona wa ajabu sana.
Mongela amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Mwanza na kukuta dawa nyingi zilizopitwa na muda wake zikiwa zimehifadhiwa huku akiwa na wasiwasi dawa hizo kurudishwa mtaani kwa watu kuuziwa bila kujua, hivyo Mongella amedai lazima kuwe na utaratibu unaoeleweka kwa hizo dawa zilizopitwa na wakati ili kuzibiti zisiweze kurudi mtaani.
Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa aliikuta gari ya kubeba wagonjwa ya Kagunguli ikiwa katika hospitali hiyo ya Nansio ambapo inasemakana imekuwepo hapo kwa zaidi ya mwaka mzima, huku watu wa Kanguli wakikosa huduma ya gari la wagonjwa na walipoolizwa viongozi walidai kuwa gari hiyo imeshindwa kwenda Kagunguli kwa sababu ya dereva.
"Mkurugenzi dereva maana yake nini naomba mtafuteni huyo dereva sasa hivi nikiwa hapa, tokea mwaka jana dereva wa Ambulance ya Kagunguli hayupo lakini nyinyi mnaniambia yupo mleteni hapa sasa nimuone, huyo dereva aje sasa hivi aondoke na diwani wa Kagunguli, diwani hata ukimuweka nyumbani kwako huyu dereva ni sawa tu, sasa dereva wa Kagunguli hospitali ya Nansio anafanya nini? alihoji Mongella
Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliendelea kusisitiza "Ile gari ya wagonjwa imeletwa hapa kule wakina mama wanakimbizwa na pikipiki wanajifungulia njiani lakini gari yao ipo hapa na sisi wote tumekaa tu, hivi akija Rais Magufuli atajua sisi ni wazima kweli? Kuna mtu atapona hapa? Kwa hiyo mimi nasema hii gari leo leo naomba iondoke hapa" alisisitiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments