-->

Header Ads

Mbunge PETER MSIGWA wa CHADEMA Akamatwa na Polisi

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa amekamatwa na Jeshi la Polisi jioni ya leo mkoani humo wakati akihutubia wananchi katika kata ya Mlandege.
 Afisa habari wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hayo wakati akiongea na mwandishi wa EATV na kusema ni kweli mbunge Peter Msigwa amekamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi mkoani Iringa.
"Ni kweli amekamatwa na jeshi la polisi wakati akihutubia wananchi kwenye majira ya 11:47 jioni ya leo, japo mpaka sasa haijasemwa sababu maalum ya kukamatwa kwake. Tumezuiliwa watu wote kumuona Msigwa hapo kituoni lakini sasa hivi tunafanya mpango wa kumpeleka mwanasheria kituoni hapo", amesema Tumaini Makene.



JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.