-->

Header Ads

KISIWA CHA ZUNIGA (4)

Na Adalgisa Kweka (4)

Kauli ya mzawa yule ilimrudisha kwenye usiku wake WA kwanza nakuanza kuzijaza nafasi alizoziacha tangu siku ile kujibu maswali yake kwamba aliyemziba macho ni huyu mzawa. Ila hakutaka mzawa yule azisomee hisia zake hivyo alionyeshwa kutokushtushwa na Kauli ile.
"Sawa mzawa"alifungua mlango nakutoka nje ambapo hakumkuta mtu zaidi ya giza lililomsabahi, hakuogopa alitembea mbele kidogo nakuangaza huku na kule hakuona mtu zaidi ya mwanga kutoka katika Majengo tofauti ya kisiwa hiko.hakujua sehemu ya afya ilipo alibaki ameduwaa asijue chakufanya alihisi yule mzawa anamchezea akili yake.akiwa anatafakari pakwenda mlango WA chumba alichotoka ulifunguka na yule mzawa Alitoka nje nakuufunga mlango alishangaa kumuona tuli bado yupo pale nje.
"Tuli Unafanya nini hapa"alimuuliza kwani hakutegemea kumkuta Yupo pale.
"sijui pakwenda"
"Hukumkuta mzawa yeyote hapa nje"
""Hapana"
" Sawa nifuate nyuma"ilikuwa ni amri. Alimfuata nyuma huku akijaribu kumlinganisha huyu mzawa na yule malaika aliyekuja kumsaidia siku ile hata hawakufanana yule alikuwa mpole hata ongea ilikuwa imejaa hekima.
"hawafanani"alijikuta akiropoka kwa nguvu kitendo kilichomfanya mzawa yule amgeukie.
"Nini?!"alimuuliza
"hamna kitu"alilaumu fikra zake ambazo zilikaribia kumponza. Yule mzawa aligeuka nakuendelea na safari. Muda simrefu walifika kwenye geti lililopambwa na nakshinakshi za dhaabu alipoangalia juu lilikuwa limeandikwa afya alijua wameshafika.wakiwa wamesimama kijana alimfungua mlango mwanzo alidhani mzawa lakini alikuja kugundua siyo kutokana na heshima aliyompa mzawa aliyekuwa naye.waliingia ndani ambapo kulikuwa na majengo Mazuri Sana ambayo hajawahi kuyaona sehemu yeyote isipokuwa dubai ambako aliwahi kwenda Mara moja Kuna Muda alihisi Yuko dubai lakini ardhi ya kisiwa ilimpigana na fikra zake.alifika karibu na chumba kama ofisi kutokana na dirisha Lake kuwa wazi ndani mwa chumba hiko kulikuwa na mmama ambaye nyuso yake ilikuwa bado ijakomaa vizuri ambaye aliwapokea.
" Kuna huyu kijana mmoja alibaki"
"aah kunachumba mule ndani ya wodi walipolazwa wajawazito"
"Sawa mzawa" aliongoza njia. Tuli alishtushwa na kauli ile du!kumbe kisiwani Kuna wajawazito,Sasa hizo mimba ni za akina nani au ni za Hawa wazawa kwamba walikuja kisiwani na wake zao.alijiuliza maswali mengi Bila kupata majibu. Safari ilikuwa si ya Muda mrefu walifika wodini nakuingia ambapo alikutana na wajawazito watatu tu wote wakiwa ni Vijana.Tuli aliwaangalia wakati anawapita, wodi ilikuwa ndogo kiasi chakumewezesha aweze kuona chumba kilichokuwa kinaongelewa na mama yule.
"Chumba umekiona ndani kina kila kitu, kesho hatutegemei kukuona katika vazi hili" aliondoka bila hata ya kwaheri au usiku mwema amakweli huku kulikuwa kisiwani kweli.Alitembea mpaka alipofika kwenye mlango wakuingia chumbani kwake alishika kitasa nakuufungua mlango wake macho Yake yalipokelewa na viti viwili vilivyotengenezwa kwa madini ya silver huku vikiwa vimechorwa maua kuvutia zaidi pamoja na meza, alipoingia nakutazama upande wake wakulia aliona kitanda kikubwa kilichotandikwa vizuri kikimpokea kwa tabasamu kwakweli chumba kilivutia sana, upande wake wakushoto aliliona kabati kubwa alilisogelea nakulifungua ndipo alipokutana na sare nyeupe zilizotundikwa kama zile za manesi alijua hilo ndilo vazi lake kisiwani hapo sehemu nyingine ya kabati ilisheheni sare hizo kwa kila aina ya rangi nakubahatika kuona nguo Moja ya kushindia pamoja na diary na peni. Alilifunga kabati lile nakurudi kuketi kitandani pake hakuelewa nini hatima ya maisha Yake Ila bado alidhamiria kutoroka.alipumzika kitandani kwa Muda mpaka alivyosikia mlango wake ukigongwa aliinuka nakwenda kuufungua alikutana na yule mama WA mapokezi akiwa amebeba sahani ya chakula.
"ukimaliza iweke nje" aliondoka. Alifunga mlango nakuketi kisha kuanza kula hakuhitaji kujua nani mpishi alichojali nikujaza tumbo lake kwasasa.alipomaliza alitii maagizo nakurudi kulala.
*_______*______*______*_____*_
Victor na saluat walifika kwenye eneo Lao ambalo lilikuwa Jengo kubwa lililovutia kuangalia walipelekwa mpaka kwenye Jengo lililokuwa kubwa kuliko yote,waliingia ndani nakuwakuta vijana wengi wakiwa wanakula wengine walikuwa wenzao waliwatambua kwa mavazi huku wengine wakiwa wale wenyeji kwani walikuwa wamevaa magwanda ya blue.
"Kajiungeni na wenzenu" Alitoa amri mzawa.waliondoka nakutafuta Meza iliyotupu waliikosa mwisho waliamua kuketi kwenye meza iliyokuwa na vijana wawili, walipoketi mzawa alikuja na sahani mbili za chakula nakuwapatia Kisha wakaanza Kula.
"tuli Atakuwa wapi"saluat alivunja ukimya bado alihitaji kujua alipo ndugu yake huyo.
"daah!au alikosea kuchagua? Lakini hapana -"
"Labda bahati haikulala upande wake"walikuwa na Mawazo tofauti ambayo yawezekana yote yalikuwa majibu ila mahojiano Yao yaliwaahangaza wale walioketi nao meza Moja,hawakuwaelewa vizuri.
"yawezekana Lakini hatutoweza kumuona Tena?"Hili ndilo lilikuwa swali lenyewe.
"hata sijui ila naimani tutamuona Tena"alijipa moyo Saluat.kisha waliendelea Kula chakula Chao
"kwanza tunalala wapi?"Saluat alikumbuka kuuliza chaajabu alimuuliza Victor ambaye walikuwa naye.
"kwa nje Kuna jengo hapo ndo sehemu ya kulala Kila chumba watu wawili wawili jinsia moja"alijibu kijana wa kiume aliyekuwa ameketi pamoja nao.
"aah Asante"alishukuru.
"nyie ni wenyeji hapa"aliuliza yule kijana Tena.swali hili lilikuja kutokana na mazungumzo yao ambayo kijana huyo alikuwa anayasikiliza.
"hapana ni wageni hapa"Saluat alimjibu kiupole Zaidi.
"ooh Sawa"waliendelea Kula raundi hii ukimya ulitawala mpaka walipomaliza Kula, kila mtu aliondoka kuelekea sehemu yake ya kulala. Vyumba vyao havikuwa tofauti na vya wengine vilikuwa vikuvutia na kama tuli walikuta nguo zakuvaa na vinginevyo. Saluat aliingia chumbani kwake ambako alimkuta mwingine ashafika alikuwa msichana mweusi ambaye sura yake ilidhihirisha kabila lake kuwa alikuwa mhaya.
"mambozako"saluat alimsalimu yule kijana mwenzie.
"poa za wewe?"alimuitikia.
"nzuri"alijibu kama ilikuwa kweli. Kulikuwa na uzuri gani kuwa sehemu ambayo huijui,uko na watu usiowajua." mimi saluat wewe Nani"alijitambulisha.
"mimi koku"
"nafurahia kukufahamu"aliendelea kuidanganya nafsi yake Kwani hakukuwa nachakufurahia hata kidogo.
"mimi pia"
Saluat alijirusha kitandani kwake nakumtakia usiku mwema koku.
Victor naye kutokana na uchovu mwingi alipofikia chumbani kwake alijirusha nakulala moja kwa moja.
*________*______*__________*_____*
Giza totoro lilitanda juu ya anga, huku kimya kirefu kikitawala kisiwa hiko.kwenye chumba walicholala wajawazito wale zilisikika kelele zilizoashiria uchungu mama,kelele hizo ndizo zilizomuamsha Tuli ambaye alikuwa kwenye usingizi wake mzuri. Kelele zile ziliendelea, zilimfanya Tuli ainuke nakuusogelee mlango wako ishara yakutaka kuufungua ndipo maneno yayule mzawa yalipomjia "usipende kuamka usiku utaja ona visivyotakiwa kuonekana" alisita nakubaki amesimama mlangoni pale huku akitegesha sikio lake aweze kusikia yanayoendelea.kelele ziliendelea lakini ghafla alisikia vishindo vya watu vikiingia alijua wazi ni wazawa ambao walikuwa wamefika hii nikutokana na viatu vyao kuwa na sori ngumu na nzito pamoja na miondoko Yao mithili ya ile ya kwata za wanajeshi.Ujio WA wazawa hao ulifuatiwa na ukimya alihisi kama Kuna mazungumzo yanayoendelea lakini hayakuyasikia ila bado hakukataa tamaa aliendelea kusikiliza akiamini kuwa Kuna kitu atakipata chakumsaidia. Akiwa pale Mara ghafla aliisikia sauti ya mzawa ikisikika vizuri.
" mtoto ameshatoka"
"ni wakike au wakike"
"wakike"
"ua Huyo"ilikuwa ni amri.
"msimuue mwanangu" alilia kwa huzuni.Tuli alikuwa akitetemeka mlangoni pale, hakuelewa kwanini mtoto yule tena Malaika alipewa hukumu ya kifo.sauti ya mama WA mtoto ilimhuzunisha sana hajawahi kuwa mama lakini kwa asilimia ndogo alielewa maumizi yake alikumbuka kilio cha mamayake alipokuwa anachukuliwa pale kwao machozi yalimtoka.
"msimuue mwanangu"aliendelea kuuomba
"KIMYA!!"ilikuwa ni amri.
"Mzawa Jose unajua chakufanya na mama"
"Ndio mkuu"
Ghafla ukimya ulitawala hakukuwa na kelele yoyote, Tuli alirudi kitandani kwake nakuketi, nguvu zilimuisha aliona kila siku yake hapo kisiwani ni yakujua siri za kisiwani ambazo hazitakiwi kujulikana isipokuwa ya Leo ilimuachia maswali mengi;kwanini walimuua yule mtoto kike? Mama wa mtoto yupo?mzawa Jose na mkuu ndo nani? Hakukuwa na jibu lililoeleweka aliamua kulala ilikujiliwazwa.
Upande WA pili usiku ulikuwa kwa saluat ambaye aliamshwa na minong'ono ya mtu aliyekuwa akiongea na simu,saluat aligeuka upande WA pili ambapo ndiko alikuwa amelala koku, alimsikia koku akilia huku kwikwi ya kilio ikimbana, alizidi kushangaa kwanini koku alilia ila kilichomshangaza zaidi ni mkono WA kushoto wakoku ulikuwa sikioni.
"Ba-ba"ilikuwa sauti ya koku iliyosheheni majonzi.saluat alishikwa na bumbuazi ni kwa vipi koku alikuwa na simu.hakuelewa kabisa, Ila hayo yote hayakuhitajika wakati huo. Saluat aliinuka nakuelekea kitandani kwa koku,ambako aliketi nakuanza kumbembeleza koku ambaye alikuwa analia Sana.
"baba yangu hawezi nisaidia, amenisahau"alilia, saluat alimbembeleza uku akiichukua simu yake nakuiweka ndani ya mto taratibu kwani alijua kuwa simu haziruhusiwi kisiwani kwani hatawalivyochukuliwa simu ziliachwa majumbani licha ya yote hakuwahi kumuona mtu na simu kisiwani  koku alikuwa WA Kwanza.
"usihofu rafiki kila kijana aliyeko huku kisiwani ana majonzi kama wewe, hauko peke yako." alimpa moyo koku ambaye alikuwa analia.
"Tuta-ondo-ka kwe-li"koku alipomaliza kuongea ghafla mlango wao ulifunguka mbele Yao waliwaona wazawa wawili mmoja akiwa amebeba bunduki kama ile ya kuwindia wanyama pori, mwingine akiwa hana silaha yoyote, wazawa wale walizidikuwasogelea, koku hakuwaona vizuri ila saluat aliwaona.
"TUNATAKA SIMU"ilikuwa ni amri iliyotoka kwa ukali nakuwatetemesha saluat na koku. Saluat alimshikilia koku kumuonyesha atulie.
"hatuna" alisema saluat kwa kujiamini Bila kujua huko kujiamini kwake kutampeleka wapi.
"TUNATAKA SIMU"amri ilitolewa tena raundi hii ilikuwa ya ukali zaidi lakini saluat alikuwa amedhamiria kuitunza siri hiyo alimjibu kuwa hawakuwa na SIMU.
"Hatuna simu, koku alikuwa ameota ndoto mbaya ndo akanshtua na mimi"alijielezea ijapokuwa hakujua itawasaidia au LA.muda wote koku alikuwa anatetemeka tu laiti angelikuwa mwenyewe angeshajitoa muhanga.
"mzawa kagua kila kitu"alisema yule mzawa ambaye alikuwa ameshikilia kitu cha moto. Mzawa alianza kukagua kitanda cha saluat walipomaliza walikuja cha koku ambapo saluat na koku walikuwa wameshainuka. Aliuinua mto WA koku nakuuugusa ambapo aliona kitu kimetuna, aliwageuzi mto ule huku akionyesha kicheko cha dharau.
"HIKI NI NINI?"Aliwauliza koku na saluat waligeukiana nakutumbuliana macho ama kweli za mwizi arobaini!!.......................... ITAENDELEA..
Kwa maoni zaidi piga 0679488502










No comments

Powered by Blogger.