-->

Header Ads

KISIWA CHA ZUNIGA (5)

 

Na Adalgisa Kweka. HIKI NI NINI aliuliza tena, waliangaliana tena bila kusema kitu ama kweli Leo ni lazima wafe!!. "hi-yo-ni-spr-ay yang-u"aliongea koku kitendo kilichomfanya saluat ashtuke kwamba ni kwanini alidanganya bora angenyamaza tu wasubiri hatua iliyokuwa inafuata. "SPREI!!"aliongea kwa dhiaka mzawa yule huku akitumbukiza mkono wake kwenye mto, muda wote roho ya saluat ilikuwa mikononi.alifanikiwa kukigusa kitu hicho alichohisi ni simu lakini sura Yake ilibadilika kidogo kitu ambacho kiliwashtua. "Kweli ni SPREI"aliiutoa mkono wake ambao ulitoka na spray ndogo iliyokuwepo kwenye kichupa kidogo cha bapa ambapo walidhania simu.saluat alishtuka hakujua ile lotion imetoka wapi wakati yeye aliweka simu kwenye mto alitaka kuamini Kuwa koku aliweka lotion ile lakini mbna na yeye alishtuka alipoona mzawa yule anakagua mto wake. "lakini mlinzi alisema amesikia sauti ya mtu akiongea na simu"aliongea yule aliyekuwa ameshika mtutu. "Atakuwa alisikia vibaya" waliondoka zao bila kuwaambia chochote kwakweli hata polisi wachunguzi walikuwa na ustaarabu kushinda wazawa Hawa.walipoondoka saluat alikimbia nakuufunga mlango na funguo haraka Kisha kurudi kitandani kwa koku. "imekuaje"alitaka kujua. "hii spray nilikuja nayo pamoja na simu na kila siku natembea nayo Jana ndo nkaiweka chini ya mto yule mzawa alipogusa Mwanzo nilihisi simu kwa jinsi ulivyoshtuka ila nilivyoangalia vizuri nkaona sio yenyewe" "Mungu mkubwa"alisema saluat maanke hakujua wangekuwa wapi Sasa hivi.saluat alichukua ule mto WA koku nakutumbukiza mkono wake ndani kabisa ndipo alupokutana na simu, aliitoa nakuiangalia,ilikuwa ni Samsung galaxy s4. "koku" aliita saluat muito wake uliashiria kukumbuka kitu. "yes" "baba yako kakwambiaje?" aliuliza kana kwamba alijua mazungumzo yaliyoendelea baina ya koku na baba yake, alihisi alichosema baba koku kingempa jibu alilokuwa analisubiria. Koku kabla yakuanza kumjibu alianza kulia jumbo ambalo lilimshangaza saluat ambaye ilimbidi ambembeleze rafiki yake huyo ambaye alikuwa anaanza kuikaimu nafasi ya Tuli. "shshhhh koku you need to be strong (koku unatakiwa uwe jasiri)lasivyo wazawa watarudi tena. Koku kila mtu hapa kisiwani anakila maumivu tena zaidi yako ila wanaishi tu kwa kufuata sheria ijapokuwa hawataki, kwahiyo rafiki yangu inabidi uwe jasiri yanamwisho" alimpa moyo koku ambaye kutokana na matendo yake alidhihirishia kila dalili kuwa alikuwa mtoto wakishua tofauti na saluat ambaye ijapokuwa kwao wana uwezo hakufanania hata robo ya uwezo huo.vibwanga vya kisiwani vilimbadilisha nakumfanya aanze kuunyemelea moyo wa idd amini taratibu akiwa na lengo lakutoka kisiwani hapo salama au majeruhi lakini si akiwa maiti. "yes I kno-w(ndyo najua) alisema koku huku akipunguza kilio chake."baba kasema hawezi kunisaidia chochote, kase-ma niishi kama hawapo-"alilia maneno ya baba yake yalimhuzunisha nakumvunja moyo sana"kasema tulivyochukuliwa hakuna hata chombo cha habari kilicho tangaza habari zozote hata wazazi walipoenda serikali za mtaa nothing happened (hakuna kilichotokea).ni siku moja tu ambapo walitangaza kama tumekufa wakaonyesha na maiti za vijana wengi, so WE ARE DEAD TO THEM!! (sisi ni  marehemu kwao)"koku alilia Sana. Maneno yake yalimgusa hadi saluat ambaye machozi ya ukimya yalimtoka huku akimbembeleza koku. "what did we do to them?(tumewafanyia nini?)"aliuliza Saluat alitamani apate jibu papo hapo. "serikali inajua kuhusu hili" yalikuwa ni maneno yaliyotoka kinywani mwa koku, maneno hayo yalikuwa ni mazito sana hata kuyaongea tu inawezekana kila mtu alihisi hivyo lakini hakuna aliyediriki kusema chochote kile. Saluat alimziba koku mdomo alihofia atasema mengi ambayo hayapaswi kusema yawezekana Kuna mtu anawasikiliza hili nalo liliutesa ubongo wa saluat. "shshh hata ukuta una masikio,uliyoongea yanatosha koku tuwaze yanayokuja" "ndyo ila sidhani kama tutatoka salama"koku alimuelewa saluat. "tutakuwa salama na tutatoka salama" alimtoa hofu koku. Mazungumzo Yao yaliwafanya wasitambue Kam kumekucha mpaka pale waliposikia milango ya watu ikifunguliwa. "duuh kumekucha twende tukajiandae" "siku ya kwanza kazini" aliongea koku kama alifurahia lakini haikuwa hivyo. Waliosha nyuso zao nakufanya usafi wa miili Yao Kisha kutinga sare zao. Walipomaliza walifungua mlango nakutoka nje ndipo walipokutana uso kwa uso na wakaka wawili ambao miili Yao ilikuwa imeshiba huku nyuso zao zikiwa zinatishia amani katakana na alama zakukatwakatwa na viwembe kwakweli walishtua kama mtu ungebahatika kukutana nao mara ya kwanza ungehisi Israeli anakutembelea siku hiyo. "kokubizaeli rwemanyika" walitaja jina ambalo lilikuwa la koku bila ubishi. Koku alimuangalia saluat kwa huzuni alishaanza kuogopa, saluat alimshika mkono kumthibitishia wako pamoja. "Mi-mi ha-pa"aliongea kwa hofu ila machozi yalishaanza kumtoka hakujua kwanini. "Twende!!"ilikuwa ni amri iliyotolewa ambayo ilimfanya koku aanze kulia huku akigoma kumuachilia saluat mkono wake. "Don't let them take me!(usiwaache wanichukue)" alisema maneno hayo kwa kuyarudiarudia kiasi chakuwafanya vijana wenzao waliokuwa wanatoka kwenye vyumba vyao wabaki wanashangaa huku wakijiuliza maswali juu ya nini alichofanya koku. "hataki kwenda tutumie nguvu" walisema wakaka wale ambao walimpiga Kofi moja koku lililomfanya aweuke Kisha walimbeba kama gunia wakiondoka naye huku koku akilia. "Saluuuuu...."alimuita saluat "Utakuwa salama"alimpa moyo hata kama hakujua nini hatima ya rafiki yake huyo,huku asijue ni kitu gani kilichomfanya aje achukuliwe. Mawazo yalimchosha nakufanya akose nguvu za kusimama badale yake aliketi chini bila kujali. Alijiinamia huku huku akiyaziba macho ishara ya kwamba yasitoe machozi. "WENYEJI!! WAHINI"ilikuwa ni sauti ya mzawa iliyosikika karibu, saluat aliisikia lakini nguvu zakusimama zilimuishia , alikuwa tiyari kwa lolote. Victor alikuwa anatoka kwa kukimbia alimuona saluat pale chini,alimfuata nakumuonyeshe mkono wake kwamba ainuke waende lakini saluat alimtingishia kichwa kuashiria hataki kwenda. Victor alimshangaa sana hakuelewa kilichomkumba lakini uso wake ulionyesha huzuni na mkato wa tamaa huyu hakuwa saluat aliyefungiwa naye kwenye kile chumba hakuwa mwenyewe. "WENYEJI WAHINI!!"Sauti ya mzawa ilisikika karibu zaidi Victor alimgusa saluat alihisi ukaribu wa sauti hiyo ungemshtua lakini hakuwa hivyo kwani pepo lililomvaa saluat halikutaka kumtoka. "Saluat sijui ni nini kimekuingia ila you have to be fine (lazima uwe salama)bado hatujajua alipo Tuli, lazima upambane" Victor alimng'oneza saluat nakuondoka eneo lile. "wewe mwenyeji hapo unatatizo gani?" mzawa yule aliuliza swali huku akizidi kutembea kufika alipo saluat. Lakini hakujibiwa swali lile zaidi ya ukimya uliotawala.alitembea mpaka alipomfikia nakumgusa saluat shavuni. "miguu yanguuu mamaaaa!"saluat alianza kulia "imefanya nini" aliuliza mzawa huyo kwa ukali "miguu yanguuu mimii uwii imekufa miguu yanguuu"alilia kwa uchungu sana kiasi chakumfanya mzawa yule amuonee huruma. "chumba chako kiko wapi?"alimuuliza huku akiangalia huku na kule kama Kuna mtu anamwangalia. "hiki hapa" alikigusa kwani ndipo alipokuwa ameketi. Mzawa yule aliufungua mlango nakumbeba saluat hadi ndani ambapo alimketisha kitandani kwake. "haya matatizo unayo tangu nyumbani" "ha-p-a-n-a"alimjibu, saluat alishtushwa na ukalimu wa mzawa yule "nilikuwa natoka nje na rafiki yangu ndo miguu-" "sawa"alimkatisha kama alijua stori nzima. Akili ya saluat ilimwambia yule hakuwa mzawa Bali ni malaika ambaye Mungu amemtumia ili amsaidie. Mzawa yule aliinuka na kwenda kuchukua heater Kisha alichota maji kwenye Bomba nakuyachemsha,yalipopata moto kidogo aliipua nakuyaweka pembeni Kisha alichukua nguo nakuanza kumkanda saluat ambaye alikuwa akipiga makelele kuashiria maumivu.zoezi Hilo lakukandwa halikuchukua Muda mrefu kwani ndani ya dakika tatu liliisha. "pumzika kidogo nakuachia hii kadi mzawa yoyote akija utamuonyesha, ukijisikia vzuri utaenda kuongea na mlinzi atakusaidia. Mzawa yule aliondoka, matendo yake yalimstaajabisha kiasi chakumfanya asahau kumshukuru. Mzawa aliondoka na igizo lake lilikuwa limeisha tiyari sasa alibaki na maswali juu ya koku, yupo wapi? Kwasababu gani? Hatima yake?.ila hakupata majibu hadi usingizi ulipomchukua kama mzoga. Nusu saa ilipita aliamshwa na sauti za mabishano alipoamka aliwaona wazawa wawili pamoja na koku, koku alikuwa amechoka huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu na nywele zikiwa timutimu, saluat aliinuka nakumsogelea koku ila wazawa wale walimstopisha. "ko-ku"aliishia kuita ila hakumjibu chochote zaidi yakumuangalia rafiki yake huyo aliyempa tumaini kwa huzuni tele. Moyoni alimuomba msamaha kwani hatoweza toka humo ndani salama. "SIMU IPO WAPI?"kibao kilimgeukia saluat alikuwa anaulizwa yeye simu ilipo hapo ndipo alipopata majibu yakinachoendelea. Akiwa ana muangalia koku aliuona mdomo wake ukichezacheza kwa shida lakini ukiwa unampa ujumbe ambao aliupata kwa shida. "sijui sijaona simu"alijitetea saluat ijapokuwa ilimuuma. "niliitupa chooni niaminini sikutaka kubaki nayo tena baa-da ya kue-le-zwa vyote , hai-ku-wa na ka-zi"alijitetea japo kwa shida lakini bado walimpiga hawakutaka kuamini alichoongea hata kidogo. Walitafuta mara ya mwisho hawakubahatika. "Hamna kitu twende naye" alisema mzawa.wakiwa wanatoka nje walipishana na mzawa wenzao akiingia. "mzawa Luka vipi" ""gudiii" "umepewa kazi haha" "Hapana nmekuja kumchukua mgonjwa" "aah Sawa Kuna mkutano wa dharura kwa WENYEJI walete vijana wake" "Sawa" Aliingia ndani nakumkuta saluat akiwa ameketi kitandani akiwaza nakuwazua mambo. "unajisikiaje?"alimuuliza "vzuri" "NIFUATE!!" alimpa amri naye alitii alianza kuongozana naye mpaka walipotoka nje, alipofika alitoa simu kitu kilichomshtua saluat ambaye aliamini wazawa hawana simu. Alimpigia mzawa mwenziye nakumuamuru alete vijana Kuna mkutano. Alikata simu nakuendeleaa na safari ambayo iliishia kwenye uwanja aliokamatwa na wenzie siku ile kwenye foleni hakujua Kuna nini. Walikuwa watu wa kwanza kufika baada ya dakika kumi vijana walifurika wakiwa wamevaa sare walipendeza,saluat Leo alikuwa yupo mbele kabisa. Kimya kilitawala ndipo alipotokea baba wa makamo akiwa amevalia jinsi kali akiwa amechomekea tisheti la khaki alikisogerea kipaaza sauti. "WENYEJI UKIKIUKA SHERIA YA KISIWA ADHABU YAKE NI KIFO KWASABABU HUFAI KUWA MZALENDO!!LEO TUTAWAONYESHA!!" aliishia hapo Kauli yake ilimfanya saluat amuwaze koku alijipa moyo kuwa kesi ya koku haikuwa kuwa kustahili hukumu ya kifo tena mbele ya kadamnasi Hapana!! Kwanza walishamuadhibu vyakutosha. Ukimya ukiwa umetawala wazawa wawili wanaingia huku wakiwa wamemshikilia mtu ambaye alikuwa Si mgeni machoni, alivyozidi kusogea mbele mtu yule ndipo alipoiona sura ya koku ambayo ilikuwa tofauti naalivyotoka kumuona masaa machache yaliyopita alikuwa msafi Hana hata tone la damu, nguo alizovalishwa zilimkaa vizuri makudhihirisha umbo lake zuri la kihaya koku alikuwa msafi ijapokuwa alifahamiana naye Jana usiku alihisi alifahamiana naye kama miaka mitatu nyuma.saluat alimchunguza rafiki yake huyo mpya kwa huzuni, wenyeji walikuwa kimya wakisikitika sana hasahasa wale waliomuona asubuhi akiwa anachukuliwa wengi walimtafuta saluat alipo kwani waliamini anaweza kujiua Masikini saluat alizidi kumuangalia koku hatimaye sura zao zilikutana,tofauti na siku zote leo alimuangalia bila kuongea na kama haitoshi alitabasamu ilikuwa ni kama maumivu na uchungu vilimzidi hivyo ilimbidi atabasamu. "what did we do to them(tumewafanyia nini).....don't let them take me don't let them take (usiwaachie wanichukue) Siku ya kwanza kazini..." maneno ya koku yalimfanya atoe machozi. Wazawa hawakujali huzuni za wenyeji wala machozi ya saluat walikishusha kitanzi nakumsogezea kistuli,kuashiria hapande mpaka hapo saluat aliona wazawa walishapania kumuua koku hawakuwa na huruma hata chembe. "kokuuu"aliita sauti haikutoka,"kokuuu kokuuu kokuuu"alijitahidi lakini haikuwezekana sauti ilishaamkauka kiasi chakuwafanya waliokaribu naye wamuonee huruma sana ingawa hawakuwa na chakumsaidia. Koku alitii sharia nakupanda kwenye kistuli kisha mzawa alimvalisha kitanzi cha hukumu, alikuwa ni yuleyule mzawa aliyekuja usiku kupekua ghafla chuki ilimvaa pamoja na roho ya kisasi alidhamiria kupanda pale Juu akamtetee rafiki yake katika hukumu hiyo, ghafla mkono ulimshika nakumvuta kwa nguvu hakuweza pingana nao kutokana na mvutaji kuwa na nguvu haswa alivutwa mpaka alipotoka nakuwaacha wenyeji wenzake. Alipomuangalia alikuwa ni mzawa kutokana na mavazi yake bila kukosea akajua ni yule mzawa Malaika,wakiwa wanatembea ghafla walisikia sauti za watu zikionyesha simanzi, saluat aligeuka nyuma kwa mbali alimuona koku akibembea alishindwa kuendelea, nguvu zilimuisha alidondoka chini kama mzigo tena mzito sana. Mzawa yule alimuangalia Kisha alimuinua nakuondoka naye, walifika hadi kwenye jengo zuri kwa Juu liliandikwa afya Kisha waliingia. Muda wote huo saluat alikuwa mithili ya bubu alihitaji mtu amtoe eneo lile la tukio na alimpata ijapokuwa bado alikuwa kisiwani. Walifika mpaka mapokezi wakapokelewa na mmama aliyempokea tuli. "anasumbuliwa na nini huyo" "presha" mzawa alijieleza ijapokuwa saluat alijua ni uongo mtupu. "ingieni ndani mpeleke chumba cha mwisho Kuna mwenyeji pale apumzike Kwanzaa. "Sawa mzawa"alimuitikia. ******************************************** Tuli aliamka akiwa bado na usingizi kutokana na mambo aliyoyashuhudia jana. Alikuja kuamshwa kisha alijiandaaa baadaa ya hapo alitoka nje ambapo alikutana na wajawazito wawili ila mmoja hakumuona moja kwa moja akajua ambaye hayupo ndiye aliyejifungua jana usiku sasa hakujua yupo wapi. "mwenyeji" aliitwa na mzawa wa kike "ndyo mzawa"alishaanza kujifunza jinsi yakuitikia wito. "Leo utakuwa na mzawa Jose wodini hapa" "ndyo mzawa" Aliitikia ijapokuwa alijua amechelewa kuamka kwani wenzie walishakunywa Chai nakuondoka Kazini.Alitoka wodini nakuenda kunywa Chai ambapo alichukua dakika tano nakurudi wodini ambapo alikutana na taarifa za mkutano ila yeye aliaambiwa abaki kwani yupo wodini anatakiwa awaangalie wajawazito. Tulialikubaliana na maamuzi aliingia chumbani kwake nakukaa alihitaji apate nguvu na ujasiri iliaende akakae na wale kina mama ilimgharimu nusu saa Zima haikuwa kesi kwani aliwaacha wamelala na mzawa Jose hakuepo. Akiwa ameketi Aliusikia mlango wake ukifunguliwa, tiyari alishajiandaa kwani alijua huyo si mwingine zaidi ya mzawa Jose ambaye alikuwa akimsubiria kwa hamu.lakini ilikuwa tofauti alipomuona mzawa akiingia huku amembeba mwenyeji, mzawa yule ambaye tiyari kwenye akili Yake alijua mzawa Jose alimshusha Saluat kitandani kwa Tuli, Saluat aliketi kitandani pale ndipo Tuli alipomuona rafiki yake huyo tofauti na siku zote Leo alikuwa mwekundu huku sura yake ikionyesha mgando wa machozi, alimsogelea rafiki yake huyo nakumkumbatia "salu-at"alitoa chozi la furaha hakuwa natumaini la kuwaona. "T-u-l--I"alilia raundi hii alianza mwanzo hakuelewa afurahi kamuona Tuli au alie kwamba koku kafa kwake yeye kifo cha koku lilikuwa ni pigo tosha.tuli hakuelewa Saluat analia kwasababu gani. "Tuli ameku-fa, amekufaa Tuli" aliongea kwa huzuni sana kwakweli alitilia huruma. "pole salu, nani kafa tena?" "amekufa namuona kwa macho Tuli, Tuli rafiki yetu Tuli" Alilia kwa nguvu sana. "VICTOR!!!"Tuli aliishiwa nguvu......ITAENDELEA......

No comments

Powered by Blogger.