-->

Header Ads

RIWAYA YA KISU BUTU

 
Giza mwororo lilitandaa katika mtaa wa korongoni huku mizinguko ya watu ikizidi kuongezeka wakiwa na haraka yakurudi majumbani mwao wakapumzike kama ilivyodesturi yao.watu walipita kimakundi wengine mmojamoja kila mtu akiwa na azimio lake kichwani wengine walikuwa wanawahi nyumbani wengine walikuwa wanawahi sehemu za starehe na wengine kwenye maombi; miongoni mwa watu hawa alikuepo binti mdogo amabaye sura yake ilionyesha hofu iliyomtawala huku miguu yake ikitembee kwa kusitasita na macho yake yakionyesha kila dalili ya kulengwa na machozi lakini hakuna aliyeweza kuyaona haya yote kwani kila mtu alikuwa na lake akilini.binti huyu alikuwa na mawazo mengi yaliyo kinzana akilini mwake lakini ilifika sehemu mawazo yalimchanganya mbaka akaamua aanze kukimbia ilimradi awahi kufika nyumbani kwao. "mtu mwenyewe tunayemsema si huyu hapaaa" alimuonyesha bintiye ambaye alikuwa ndo amefika. "wewe mtoto ulkuwaa wapi?hayo mafundisho ya leo yalikuwajee?”aliulza baba wa binti kwa kufoka.binti alikuwa anatetemeka mithili ya mwizi ambaye arubaini yake ilikuwa imewadia. "we siti baba yako si anakuongeleshaaa alafu..(kama ameona kitu kipya kwa mwanae) ilo begi la nani kwanza?"mama wa binti huyo anayeitwa siti alianza kumtilia shaka mwanaye kwa wakati huo. "mama hili begi kuna mwanafunzi alilisahau kanisa-ni,mwalimu ndo akaniambia niendoke na-lo" "kwanini mwalimu akwambie wew wakati yeye yupo na hiyo ndo kazi yake kama kuna bomu je!!" aliongea kwa kufoka ,siti hakuwahi kumuona baba yake katika hali hile lakini kauli ya mwisho ya baba yake ilimshtua sana kwani binafsi hakujua nini kilikuwamo katika begi hilo ambalo hata mazangira yaliyopelekea begi hilo kuwa mikononi mwake yalikuwa ni siri yake . "hapana mwalimu alisema yeye anaenda mbali kidogo atalipitia kesho baba ni yule madama stella"ilimbidi adanganye kwani hakuwa na namna nyingine tena tiyari alishaanza na uongo hivyo ilimlazimu kusalimu amri nakuwa muongo milele. "kumbe madam stella haina shidaa ebu nenda ndani ukaandae meza tuje tule"alisema mama yake kesi yakuchelewa kwa siti ilisahaulika,siti aliingia ndani na nakuandaa meza kisha aliwaita wazazi wake wakala na kwenda kulala.siti akupata usingizi kutokana na tujkio alilolishuhudia.siti aliinuka na kwenda kulifuata begi eneo alipoliweka aliazimia kujua kilichopo mule ndani ,alilichukua nakuanza kulifungua alipopenyeza jicho lake kutazama kilichomo ndani alihisi mkono ukimgusa kwenye bega lake siti alistuka alipogeuka alikutana uso kwa uso na sura ya mama yake. ITAENDELEA..                                                                   usikose kufuatilia riwaya hii kila jumatano na ijumaa.

No comments

Powered by Blogger.