MANARA AMTAMBULISHA NIYONZIMA RASMI LEO.. ASEMA HAYA.
Msemaji mkuu wa timu ya Simba, Haji Manara leo amethibitisha rasmi kuwa mchezaji wa zamani ya Yanga, Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba.
Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari katika uzinduzi wa Simba day, amesema klabu ya Simba washamalizana na Niyonzima na Jumamosi siku ya Simba day atakuwepo na kutambulishwa rasmi.
Huku akiongea kwa tambo, Manara amesema Niyonzima ana thamani ya wachezaji 10 wa Yanga akitupa dongo hilo kwa watani wake.
Siku ya Simba day pia kutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Sports Rayon kwa ajili ya burudani ikienda sambamba na utambulisho wa jezi zao mpya.