ZIJUE NDOA ZA MASTAA WA MAREKANI ZILIZODUMU KWA MUDA MFUPI ZAIDI.
ii ndio orodha ya ndoa za mastaa wa marekani zilizodumu kwa muda mfupi zaidi.
1)Zsa Zsa Gabor na Felipe De Alba
Kabla ya kuolewa na Felipe mwanamama huyu Zsa Zsa aliolewa mara 8 na kuachika na ilipofika mwaka 1983 aliolewa tena kwa mara ya tisa.Lakini ndoa yao ilidumu kwa siku moja tu na kutangazwa kuwa ndoa hiyo imevunjwa kwasababu bado alikua hajapewa talaka na mume wake wa zamani.
2)Eddie Murphy na Tracey Edmonds
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa mwaka 2008 kipindi wakiwa na urafiki na mapenzi mazito ilidumu kwa wiki mbili tu na baada ya kuona tofauti zao wakaamua kuvunja ndoa yao .
3)Kim Kardashian na Kris Humphries
Kim kardashian ambaye sasa ni mke wa rapa Kanye West aliwahi kuolewa mwaka 2011 na mchezaji wa kikapu nchini marekani Kris Humphries na ndoa yao ilidumu kwa siku 72 tu na kuvunjika.
4)Nicholas Cage na Lisa Marie Presley.
Lisa ni staa ambaye aliwahi kuwa mke wa marehemu Michael jackson ambao waliachana mwaka 1996 na mwaka 1999 Nicholas Cage na Lisa wakaanza mahusiano ya kimapenzi.
Mwaka 2002 wapenzi hawa walifunga ndoa lakini ndoa yao ilidumu kwa siku 108 tu na kupeana talaka.
5)Jennifer Lopez na Cris Judd
Jlo alikutana na Cris Judd ambaye ni densa mwaka 2000 na mwaka 2001 mastaa hao walifunga ndoa baada ya kuwa na mahusiano kwa takribani mwaka mzima. Lakini ndoa yao ilidumu kwa mwaka mmoja tu na kuvunjika mwaka 2001 mwezi wa 6.
No comments